Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu maalum ya familia duniani iliyoadhimishwa jana ambapo kauli mbiu ni 'Elimu na Malezi Bora kwa Ustawi wa Watoto'. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Watoto, Emmanuel Burton. (Picha na Mroki Mroki).
****************
Na
Halima Mlacha, Dodoma
KATIKA
kuadhimisha Siku ya Familia Duniani, Serikali imewataka wazazi kuhakikisha
wanawajibika ipasavyo katika malezi ya watoto wao, ili kuzuia jamii ya
watanzania kuwa na watoto na vijana wanaojiingiza kwenye matumizi ya dawa na
uhalifu.
Aidha,
imewaomba viongozi wote wa dini nchini kuhakikisha wanatumia dakika chache
katika mahubiri yao, kuzungumzia malezi bora ya watoto ili kupunguza kasi ya
ukatili wa watoto na kuondokana na kizazi cha watoto watukutu na wahalifu.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu maadhimisho hayo, Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema wizara
hiyo imebaini pamoja na kuwepo kwa sababu nyingine zinazowafanya vijana
kujiingiza kwenye uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya, lakini ukosefu wa
malezi bora ya wazazi au walezi nao pia unachangia.
“Tunawaomba viongozi wa dini watumie japo
dakika tatu kwenye kila mahubiri yao kuzungumzia malezi bora, tunaamini nguvu
ya viongozi wa dini wakilisemea hili familia zitakuwa bora hali hii itasaidia
sana kupunguza matatizo yanayowapata watoto wetu,” alisema Mwalimu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment