Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, 15 May 2017

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA HII LEO

 BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea na Mkutano wake wa Saba wa Kikao cha 25 cha Bunge la 11 mjini Dodoma hii leo ambapo mbali na maswali na majibu kipindi cha asubuhi pia Wabunge walipata fursa ya kuendelea na mjadala wa randama ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
 Wabunge wa Viti Maalum kutoka kushoto, Dk Immaculate Semesi  Oliver Semuguruka na Shally Raymond wakisalimiana nje ya uklumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
 
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura (kulia) akiwa na Mbunge wa Viti Maalum, Rhoda Kunchela wakiingia Bungeni mjini Dodoma
 Mbunge wa Viti Maalum, Mariamu Ditopile Mzuzuri, akiuliza swali kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bungeni Mjini Dodoma leo ambapo alitaka kujua kama serikali ilifanya utafuti na kugundua ni kwa kiwango gani Shisha inamadhara makubwa kulilo uvutaji sigara nchini.
Mbunge wa Viti Maalum, Latifa Chande akiuliza swali alilolielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara bungeni mjini Dodoma jana ambapo alitaka kujua ni lini serikali itajengwa kiwanda cha kukamulia ufuta wilayani Liwane mkoani Lindi. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.

 Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (kushoto) na Mbunge wa Mbinga Vijijini Martin Msuha wakiingia Bungeni Mjini Dodoma
 Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo akitoa ufafanuazi wa maswali yaliyoelekezwa katika wizara yake Bungemi mjini Dodoma
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa Bungeni mjini Dodoma jana. Mbele yake ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Mchemba
 Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akizungumza jambo na Mbunge wa Viti Maalum Upendo Peneza bungeni Mjini Dodoma leo.
 Mbunge wa Muhambwe  Atashasta Nditiye akiuliza swali Bungeni mjini Dodoma
 Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bungeni mjini Dodoma leo.
 Wanafunzi kutoka TIA wakiwa Bungeni mjini Dodoma
 Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akiwa Bungeni mjini Dodoma leo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment