Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 15 May 2017

SERIKALI KUDUMISHA MATIBABU YA UZAZI PINGAAMIZI.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumzxa na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika  leo jijini Dar es salaam.

Waandi wa habari  wakimsikiluliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel  Massaka,Globu ya Jamii.
*****************
SERIKALI  yaja na mpango mkakati wa kudumisha matibabu ya uzazi pingamizi ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano  nchini Tanzania.


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati waa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika jijini Dar es salaam.


“Huwezi kutoa huduma bora na salama  ya uzazi pingamizi bila kuwa na wataalamu wa ganzi ili kufanywa upasuaji usio na maumivu hivyo katika mkutano huu tunapanga kuwa na wataalamu wengi wa huduma hiyo ili kutoa huduma bora nchini.


Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa licha ya kudumisha matbabu ya uzazi pingamizi pia Serikali imejidhatiti kujenga vituo vya afya vinavyotoa huduma hiyo kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.


Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mkutano huo unalenga kutoka na malengo ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa mahututi pamoja na kutoa huduma ya ganzi kwa wanaohitaji kupasuliwa.


Mkutano huo ulioandaliwa na Chama cha Wataalam Wa Ganzi nchini (SATA) umeudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Sweden,Cameroon, Marekani , Tanzania  ili kuweza kujua mchango wa kupunguza vifo vya wajawazito kutokana na huduma ya ganzi.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment