Na Daudi Manongi-MAELEZO,
DODOMA.
Serikali kupitia Mamlaka ya
Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230 kwa
kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo wa
kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la
Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Engelbert leo Bungeni.
“Mtambo huu umesaidia Mamlaka
ya Mawasiliano nchini kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano
pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya
Mawasiliano Duniani kote”,Aliongeza Ngonyani
Aidha kati ya pesa izo bilioni
56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni 6,028,081,599
zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia
tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya hapo kahukuwa na
mapato hayo.
Amesema mtambo huu umeiwezesha
TCRA kuwa na uwezo wa kusimamia mawasiliano ya simu za Kimataifa na zile za
mwingiliano,pia mtambo huo umesaidia kudhibiti mawasiliano ya Simu za ulaghai
za kimataifa na kusimamia ubora wa mitandao katika kutoa huduma bora kwa
wananchi,kudhibiti namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano nchini pamoja na
usimamiaji wa miamala ya fedha inayopita
katika mitandao ya simu hapa nchini.
“Aidha pamoja na mafanikio
hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na kujiridhisha
juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za
mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki
kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea”Aliongeza Ngonyani.
Aidha Serikali itaendelea
kuwajengea uwezo wataalamu wa TCRA ili waweze kuendana na kasi ya ukuaji wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususani katika eneo hili la kuchakata
taarifa mbalimbali za huduma za mawasiliano zinazopatikana kutoka kwa watoa
huduma ili kuweza na kujiridhisha juu ya mapato yote.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment