Na Alexander Sanga,Shinyanga
Shauri la Mgogoro wa kikazi baina chama cha wafanyakazi wa mgodini mkoani Mara(NUMET) na mgodi wa North Mara itatolewa maamuzi Desemba 29 mwaka huu .
Shauri hilo Namba CMA/MUS/ 201/2017 ipo chini ya mwamuzi wa tume ya usuluhishi uamuzi(CMA) Shinyanga, Kiliani Nembeka.
Akizungumza baada ya kusogezwa mbele shauri hilo, wakili wa kujitegemea upande wa mwombaji Galati Mwentembe alisema wameamua kufika hatua hiyo kufuatia upande wa wafanyakazi kukwamisha mchakato wa ubinafsishaji hali iliyopelekeaa kukimbilia kwenye hatua ya usuluhishi.
“North Mara imefikia hatua ya kubinafsisha kitengo cha ulinzi na kimsingi hatua hiyo itawagharimu baadhi ya wafanyakazi kwa kuachishwa kazi na kimsingi kisheria lazima muingie makubaliano kati ya kampuni na waajiri ambapo wenzetu(NUMET Mara) hawakuwa tayari na ndo tukachua hatua hii ya usuluhishi,” alisema Galati
Akielezea zaidi sababu kubwa ya kutaka kubinafshisha kitengo cha ulinzi,Galati alisema shughuli za ulinzi zinahitaji ulinzi wa hali ya juu na mgodi wao ulikuwa ukivamiwa na kuibwa kwa mali mbali.
Galati alisema ni wasi mgodi wao utapunguza wafanyakazi 136 ambao ni walinzi wa mgodi huo.
Kwa upande wake wakili wa kujitegemea upande wa mjibu maombi, Ambrosi Malamsha alisema wateja wake walikuwa tayari kuendelea na mchakato wa kubinafsisha kitengo hicho lakini kuna taratibu zilikiukwa hali iliyopelekea kuona mchakato huo ni batili.
Malamsha alisema mchakato wanaotaka kufanya North Mara sio sawa kwa kuwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi wanatakiwa kuondoka wote na kuomba kazi upya.
Malamsha alisema watapeleka hoja za mwisho Disemba 22 mwaka huu.
Mazungumzo ya ubinafishaji ya kitengo cha wafanyakazi baina North Mara na NUMET yalianza Julai mwaka huu lakini Septemba 29 yalivunjika ndipo wakafishana tume ya usuluhishi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment