Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, 3 April 2017

BINTI WA MIAKA 16 ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJITOSA BAHARINI KUTOKA KATOIKA BOTI YA MV KILIMANJARO


Waokoaji kutoka katika Boti ya Mv Kilimanjaro wakijaribu kumuokoa Binti wa miaka 16 aliyetambulika kwa jina la Huzaima Salum Abrahman aliyejirusha Baharini wakati Boti hiyo ya mwenda kasi aliyokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Unguja visiwani Zanzibar hii leo.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MSICHANA Huzaima Salum Abrahaman (16), amenusurika kifo baada ya kujirusha baharini katika boti inayokwenda kwa kasi ya Mv Kilimanjaro akitokea jijini Dar es Salaam kwenda Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Hassan Nassir Ali aliyethibitisha kutokea kwa tukio hilo, alifafanua kuwa tukio hilo lilitokea jana asubuhi.

Kamanda Ali alisema chanzo cha msichana huyo kujitosa baharini hakijafafahamika kwa sasa na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

“Tunachunguza kujua huyu msichana huyu kwa nini alifanya jaribio la kujiua, tukio ambalo ni la kwanza kutokea mwaka huu,” alieleza Kamanda Ali.

Video iliyoonekana kwenye mitandao tofauti ya kijamii inamuonesha msichana huyo akiwa anaokolewa na wazamiaji watatu ambao walisaidiwa na mabaharia wa boti hiyo takribani watano, kumtoa kwenye maji mwanadada huyo.

Hata hivyo, pamoja na kuokolewa, alionekana akilia kwa sauti ya juu huku waokoaji wake waliokuwa wakijitahidi kumvutia kwenye boti ambako walimhifadhi sehemu salama.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment