Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Manyara,Venance Msafiri (kulia) akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Francis Assenga (kushoto) kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga (kushoto) akitambulisha
mikopo na huduma zinazotolewa na Benki yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera
kuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera akisisitiza umuhimu wa TADB kwa mkoa wa Manyara.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akisisitiza utayari wa Benki yake kuwekeza
mkoani Manyara.
************
Na mwandishi wetu, Manyara
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera ameiomba Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania
(TADB) kwenda kuwekeza mkoani humo kwa kuwapatia kuwapatia mikopo na
mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mkoa huo.
Akizungumza wakati wa mazungumzo na ugeni kutoka TADB uliomtembelea Ofisini kwake, Mhe. Bendera
amesema mkoa wa Manyara una fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo kulinganisha na mikoa mingini nchini.
“Mkoa wa Manyara una fursa nyingi sana ambazo Benki inaweza kutoa mikopo ambayo nina uhakika
itarudishwa kwa wakati kwa sababu watu wa Manyara ni waaminifu sana,” alisema Mhe. Bendera.
Akizungumza
na Mhe. Bendera, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
amesema
Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili
kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza
mapinduzi katika
kilimo nchini.
Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta za kilimo na mifugo ni sekta za kipaumbele ambazo zinazopatiwa
mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa sekta hizo nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta hizo ili kuongeza
tija sekta hizo.
“Benki
inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka
Miwili (2)),
Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na
Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).
“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” aliongeza.
TADB
ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu
mkubwa wa upatikanaji
wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa
unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha
kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye
mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti
magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo
na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment