Msemaji wa Jeshi la Polisi ACP-Advera Bulimba
JESHI la Polisi
nchini li limetoa ufafanuzi kuwa, Fomu ya Polisi namba 3 ijulikanayo kama PF.3 hutolewa kwa mtu baada ya Polisi kupata taarifa kutoka
kwa mlalamikaji au muathirika kwa
matukio yenye madhara mwilini, ajali au
matukio yenye kuleta mashaka kuhusu vyanzo vyake kama vile kipigo,
kujeruhi, ubakaji, kulawiti, kunywa sumu
na mengineyo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP, Advera Bulimba katika katika taarifa yake kwa umma amesema kuwamatumizi ya PF3 bado ya naendelea na ni yalazima kwa mujibu wa sheria hivyo inapaswa kutumika kwa kila tukio.
"Ieleweke wazi kwamba matumizi ya PF3 ni ya lazima na
yanaendelea kama kawaida kwa mujibu wa
sheria, fomu hiyo inapaswa kutumika kwa kila tukio la aina tajwa hapo juu ili muathirika aweze kupata matibabu katika vituo vya Afya
na hatua za kiupelelezi kwa Jeshi la
Polisi ziweze kuendelea,"alisema ACP Bulimba.
ACP Bulimba amesema Katika mazingira mengine hali ya muathirika
inaweza kuwa mbaya, hivyo, huduma za
kuokoa maisha (huduma ya kwanza) zinaweza kuendelea kutolewa wakati watoa huduma ya afya wakiijulisha Polisi ili kuharakisha upatikanaji wa PF 3.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment