Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 1 July 2017

MAJALIWA:HAKUNA MSAMAHA KWA WANAOUIBIA USHIRIKA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia  katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba (katikati) na Naibu Waziri wa Kilimomo, Mifugo na Uvuvi, Tate William Ole- Nasha baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma  kuhutubia katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma
 Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa ikiongoza maandamano katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma
 Baadhi ya washiriki wa  kilele  cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma Julai 30, 2017 wakiandamana
 Waziiri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli mbalimbali za korosho katika wakati alipotembelea banda la Ushirika wa Ruangwa, Nachingwea Liwale Cooperative Union (RUNALI) Limited  katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma Julai 30, 2017. Kushoto  kwake ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Convenant, Sabetha Mwambenja.
 ***************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitamsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhilifu wa mali za fedha za Ushirika nchini.

“Kwa Serikali hii ya awamu ya Tano tutachua hatua kali kwa wezi wa mali na fedha za ushirika na tunaendelea kufanya usafi wa wabadhilifu hadi tupate viongozi waadilifu,”.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai Mosi, 2017), katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD), iliyoadhimishwa kitaifa mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Amesema miongoni mwa changamoto zinazoukabili Ushirika nchini ni pamoja na wizi na ubadhilifu wa rasilimali za Ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wasiokuwa waaminifu.

 Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine ni baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika kutoheshimu miongozo ya vyama vyao na kujifanyia mambo kwa maslahi yao binafsi.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake na kuweka mazingira rafiki ya kustawisha Ushirika nchini ili kutoa fursa ya Ushirika kushamiri na kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi yao.

“Haikubaliki hata kidogo kuona sekta hii inayosadifu maisha ya Mwafrika hamnufaishi ipasavyo , hivyo naelekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ihakikishe kuwa vyama vya Ushirika vinaendeshwa kisayansi na kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Pia amezielekeza Kamati za Ushauri za Mikoa na Wilaya nchini, ziingize agenda ya Maendeleo ya Ushirika kama moja ya agenda muhimu inayopaswa kujadiliwa na kuwekewa maazimio ya utekelezaji. Pia wawe na takwimu za vyama vya Ushirika na Wanaushirika.

Hata hivyo Waziri Mkuu amezielekeza mamlaka zote zinazohusika na Ushirika nchini zijiwekee malengo yanayopimika ya namna ya kuboresha sekta ya Ushirika.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameelekeza kwamba masuala yote yanayohusu Ushirika wa kilimo nchini lazima yaratibiwe na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Aidha, Waziri Mkuu amezielekeza Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zifanye mapitio kubaini elimu na ujuzi katika ngazi zote za Ushirika kwa ajili ya kuwaandalia kozi za muda mfupi za kuongeza ujuzi au kubainisha aina ya watumishi wanaohitajika kwenye sekta hiyo.

Pia amewaagiza Maofisa Ushirika nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri uchanguzi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) na kuwaondoa wagombea wote waliowahi kuwa viongozi, ambao waliondolewa madarakani kutokana na ubadhilifu wa mali na fedha za Ushirika.

Awali, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alisema wizara itaendelea kusima na kuchukua hatua kwa viongozi wote wa vyama vya Ushirika watakaobainika kufuja mali na fedha za Ushirika.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment