Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 1 July 2017

RAIS MAGUFULI AAHIDI MAZINGIRA BORA ZAIDI YA UWEKEZAJI NCHINI

RAIS John Magufuli amefungua maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) leo na kuahidi kuendelea kutoa mazingira bora ya uwekezaji nchini. Anaandika Mroki Mroki.

Rais Dk Magufuli amewahakikishia wadau wa maendeleo zikiwemo kampuni za biashara za ndani na nje ya nchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji nchini na ametoa wito kwao kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika viwanda.

Rais Magufuli amesema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Maonesho hayo ya 41 ya Biashara maarufu kama sabasaba yaliyoanza Juni 28 mwaka huu na kutarajiwa kumalizika Julai 13 mwaka huu baada ya kuongeza juma moja.

Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam ambapo
jumla ya kampuni 515 kutoka nchi za nje 30 na kampuni zaidi ya 2,500 za ndani ya nchi zinazoshiriki.

Dkt. Magufuli ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeanza kuchukua hatua madhubuti za kuboresha uwekezaji katika viwanda ikiwemo masuala ya kodi na kuongeza uzalishaji wa umeme na ameahidi kuwa wote watakaokuwa tayari kujenga viwanda watapata ushirikiano wa kutosha kufanikisha azma hiyo.

“Tunapanua mradi wa Kinyerezi I na tunajenga Kinyerezi II na III, hizi zote zitatupatia Megawatts 600 za umeme, na pia tumeamua kutekeleza mawazo ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya kujenga mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), mradi huu utatupatia Megawatts 2,100",alisema Rais Magufuli. 

Aliongeza kuwa “Ni mradi mkubwa na tumeamua kuanza kuujenga kwa kutumia fedha zetu, najua watu watajiuliza fedha tutapata wapi, nasema tutajenga” 

Rais Magufuli alisisitiza kuwa licha ya manufaa ya kupata umeme pia bwawa litakalojengwa litatumika kwa uvuvi, maji ya wanyamapori na Kilimo.

Rais amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuongeza muda wa maonesho hayo kwa siku 5 zaidi ambazo zitaishia tarehe 13 Julai, 2017 ili Watanzania wapate muda mwingi zaidi kutembelea na kujifunza teknolojia, ujuzi na mbinu mbalimbali za biashara.

Aidha amezipongeza kampuni 515 kutoka nchi za nje 30 na kampuni zaidi ya 2,500 za ndani ya nchi zinazoshiriki katika maonesho hayo makubwa Afrika Mashariki na Kati na ametembelea baadhi ya mabanda ya kampuni hizo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment