Na Daudi Manongi-MAELEZO,
DODOMA.
SERIKALI kupitia Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa itaendelea
kuhamasisha Halmshauri zote nchini
kununua viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua viluilui vya mbu waenezao
Malaria vinavyotengenezwa na kiwanda cha Biotec product cha Kibaha.
Hayo yamesemwa leo Bungeni na
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dk
Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la
Mbunge wa Gando, Othman Omar Haji.
“Viuadudu hivi bimeanza
kutengenezwa kuanzia mwezi Desemba 2016 na kwa sasa uhamasishaji huu
unaendelea na endapo viuadudu ivi
vitatumiwa vizuri vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha maambukizi
ya Malaria nchini”,Alisema Mhe.Kigwangalla.
Aidha amesema Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano na Serikali ya Cuba imeendelea
kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo pamoja na Sekta ya Afya tangu mwaka
1986 mkataba uliposainiwa kati ya Serikali hizi mbili.
Kupitia mkataba huo Serikali
ya Tanzania imekuwa ikipokea madaktari bingwa kutoka Cuba ambao wamekuwa
wakifanya kazi katika Hospitali za Muhimbili,Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya
, Hospitali Tumbi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Mbali na hayo amesema kuwa
Madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kibingwa kwa wananchi na
kuwajengea uwezo madaktari wanaofanya nao kazi katika Hospitali hizo.
Aidha kwa kushirikiana na
kampuni ya Labiofarm ya Cuba,Serikali imeweza kujenga kiwanda cha kutengeneza
viuadudu ivyo na Serikali ya Cuba imeleta wataalamu.
Kiwanda icho cha Biotec cha
kibaha kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 2.5 za viuatilifu vya kuua viluilui vya mbu waenezao Malaria kwa mwaka.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment