KATA ya Iponya imevuka lengo la uandikishaji watoto wenye
umri chini ya miaka mitano kwa ajili ya kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kwa zaidi ya
watoto 900 sawa na 154.7%
Kauli hiyo ilitolewa na mratibu
wa zoezi la usajili wa watoto chini ya
umri wa miaka mitano wa wilaya ya Mbogwe, Fredrick Chotamasege, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya hali ya
uandikishaji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
aliyefanya ziara ya ufuatiliaji katika kata ya Iponya.
“Kata ya Iponya imefanikiwa
kuvuka lengo katika zoezi la uandikishaji watoto chini ya umri wa miaka mitano zoezi linaoendeshwa na wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA). Kata ya Iponya iliwekewa lengo la kuandikisha watoto 1,806
lakini hadi kufikia tarehe 16/05/2017 ilikuwa imeandikisha watoto
2,794” alisema Fredrick.
Aliongeza kuwa usajili huo ni sawa na ongezeko la
watoto 988 waliosajiliwa sawa na 54.7%.
Pamoja na mafanikio makubwa
ya zoezi
hilo,zipo changamoto za
mawasiliano ya mtandao wa Tigo unaotumika kutuma takwimu hizo. Aliongeza kuwa mtandao huo umekuwa ukitumia muda mrefu
kutuma majina na hivyo kusababisha kuwa na takwimu tofauti kati ya zile zilizopo
kwenye vitabu na zile za kwenye mtandao wa RITA.
Haya yalielezwa wakati Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Mbogwe, Elias Kayandabila, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya zoezi la
uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika kata za Masumbwe na
Iponya wilayani Mbogwe.
Hata hivyo, baada ya Mkurugenzi, Kayandabila kuridhika na hatua za uandikishaji aliwaagiza waratibu wa zoezi
hilo kwenye kata kufanya ukaguzi wa vitabu (physical verification) ili kupata
takwimu halisi kama alivyoshiriki yeye mwenyewe kwenye kata ya Iponya na Masumbwe
,ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tatizo la kimtandao.
Kayandabila alisisitiza
kuwa “ Mbogwe ni miongoni mwa wilaya
zenye mwingiliano wa watu na nchi jirani, hivyo amewaagiza waratibu wa zoezi kuorodhesha watoto wote ambao wanakuja bila
kadi ya kliniki au tangazo la kuzaliwa ili waweze kufuatiliwa na kujiridhisha
kama kweli wamezaliwa hapa nchini licha ya kupata barua za utambulisho kutoka
serikali ya kijiji".
Mkurugenzi amewasihi wazazi
wa watoto kuwa na makubaliano ya majina
kabla hawajaenda kwenye vituo vya kusajilia ili kupunguza changamoto
iliyojitokeza kwa baadhi ya wazazi kutoelewana juu ya majina ya watoto na hivyo kusababisha
kuharibika kwa vyeti .
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment