Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 7 April 2017

WASANII WA MUZIKI WAKUTANA KUZUNGUMZIA KUTOWEKA KWA MWENZAO ROMA MKATOLIKI

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamekutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadilj,mustakabali wa msanii mwenzao Ibrahim Mussa maarufu kama Roma, Moni Centrozone pamoja na wenzao wawili wanaodaiwa kutekwa na watu wasiofahamika.

Wengine wanaodaiwa kutekwa na watu hao wasiofahamika ni pamoja na prodyuza wa studio ya Tongwe Recods, Bin Laden au Belo pamoja na kijana aliyetambulishwa kwa jina la Emma ambaye ni mfanyakazi wa mama mzazi wa mmilkki,wa studii hiyo, Junior Makame maarufu kama J Murder.

Aidha wasanii hao pia wamewataka wananchi kuacha kuwatuhumu viongozi wa serikali na wanasiasa kuhusika na kutekwa na akina Roma na wenzake, kwakuwa hata wao hawajui ni watu gani waliohusikabna kuwateka wasaniibhao.

"...sisi wenyewe hatujui kama ni serikali, hatujui kama ni watu wabaya, hatujui ni watu wa aina gani, hii ni kesi tofauti ya kesi kama ya Nay (Wa Mitego) ambaye tulikuwa tunajua yupo kituoni Morogoro muda huu unaletwa Dar...watu waache kuwasotea watu video ambao hatuwajui," amesema mwanamuziki Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment