Friday, 31 March 2017
PROF.KABUDI ASEMA SASA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO KUANZA KUTOLEWA KATIKA KANDA
Friday, March 31, 2017
SIKIA ALICHOSEMA NEY WA MITEGO KUHUSU POLISI ALIPOKUTANA NA WAZIRI MWAKYEMBE MJINI DODOMA
Friday, March 31, 2017
WANAWAKE WASHIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI MASOKONI JIJINI DAR ES SALAAM
Friday, March 31, 2017
Mwenyekiti wa Soko la Gezaulole lililopo Kiwalani Bomu bomu, Muhidin Waziri 'Ndolanga' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu changamoto iliyokuwepo katika soko hilo juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo hivi sasa vimedhibitiwa baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG). Kulia ni Mwezeshaji wa Kisheria wa soko hilo.
Mwezeshaji wa Kisheria katika soko hilo, Amina Mussa akizungumza na wanahabari.
Mfanyabiashara katika soko hilo, Zena Mohamed akielezea wanawake kupiga hatua ya maendeleo baada ya kupata mafunzo hayo yaliyotolewa na EfG.
Wanawake wakipata mahitaji mbalimbali katika soko hilo.
Mteja akinunua bamia. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Thursday, 30 March 2017
KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YAMWAGIZA MSAJILI HAZINA KUTAFUTA BODI YA TCAA
Thursday, March 30, 2017
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama amewaambia waandishi wa Habari
Mjini Dodoma leo baada ya kumaliza kikao hicho kuwa, Kamati yake imepokea
ripoti ya utendaji wa TCAA lakini wameshindwa
kuijadili baada ya kubaini kuwa watendaji wakuu wote wa mamlaka hiyo hawapo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PIC, Albert Obama akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Lolencia Bukwimba na Katibu wa Kamati hiyo wakiendelea na kikao mjini Dodoma leo.
KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa
Mitaji ya Umma (PIC) imegoma kujadili taarifa ya Malaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) hadi pale Msajili wa Hazina atakapo hakikisha kuwa Mamlaka hiyo inapata Bodi.
Mwenyekiti wa Kamati wa
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama amewaambia waandishi wa Habari
Mjini Dodoma leo baada ya kumaliza kikao hicho kuwa, Kamati yake imepokea
ripoti ya utendaji wa TCAA lakini wameshindwa
kuijadili baada ya kubaini kuwa watendaji wakuu wote wa mamlaka hiyo hawapo.
Obama alisema kuwa TCAA
wametumwa wawakilishi tu, lakini kuanzia Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi wa
Mamlaka ambao kimsingi ndio watendaji na ambao wanaidhinisha miradi hawapo.
“Kama Mkurugenzi wa TCAA
na Mwenyekiti wa Bodi hakuweza kufika basi walau tungekuwa na hata na Katibu
Mkuu basi wa Wizara,” alisema Obama.
Alisema Kamati imemwagiza
Msajili wa Hazina kwenda kuhakikisha uongozi wa Bodi na Menejimenti unakamilika
ndipo wataomba kwa Spika wapangiwe kujieleza.
Kutokana na kushindikana
kujieleza Kamati imeahirisha kuwapa nafasi kujieleza wajumbe watatu waliokuwapo
ambao nao wana kaimu nafasi zao.
“Kamati hii ni mtambuka hivyo
bila kuwapo waidhinishaji miradi na watekelezaji, ni vigumu kutoa maagizo kwa
wajumbe badala ya viongozi,”alisema Obama.
KAMATI YA BUNGE YA PIC YAGOMEA KUJADILI TAARIFA YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TCAA
Thursday, March 30, 2017
Wednesday, 29 March 2017
CCM YAPITISHA 12 KUWANIA UBUNGE KATIKA BUNGE LA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI (EALA)
Wednesday, March 29, 2017
Dk.Abdallah Hasnu Makame
Fancy Nkuhi
Adam Kimbisa
Zainab Kawawa
Charles Makongongo Nyerere
********
KAMATI Kuu
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imepitisha majina 12 ya Wanachama wake walioomba
kugombea Ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Jumla ya
wana CCM 450 waliomba ridhaa ya Chama kupitishwa kuweza kuwania ubunge wa Bunge
la Afrika Mashariki (EALA) ambapo Wabunge wa chama hicho walipiga kura jana
kuchuja majina hayo.
Hii leo majina
12 yaliyopitisha na Kamati Kuu yamewekwa hadharani baada ya kufanyika mchujo
Waliyopitishwa
na Kamati Kuu na sasa wanasubiri kupigiwa kura na Bunge Aprili 4, mwaka huu ni Zainab
Kawawa, Happines Lugiko, Fancy Nkuhi, Happines Mgalula, Ngwalu Jumanne Maghembe,
Adam Kimbisa, Anamringi Macha, Charles Makongoro Nyerere, Mariam Usi Yahya, Rabia
Abdalh Hamid, Dk. Abdallah Hasnu Makame na Mohamed Yusuf Nuh.
SIKILIZA HAPA ALICHOKISEMA MKUCHIKA BAADA YA KAMATI YA BUNGE KUMHOJI PAUL MAKONDA
Wednesday, March 29, 2017
MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AZINDUA ZOEZI LA UTHAMINI
Wednesday, March 29, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Ezekiel Odunga akizungumza na wananchi wa kata ya Farkwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la uthamini mali ili kupisha ujenzi wa bwawa la Farkwa.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma akiongozana na baadhi wa Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Wataalamu wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Uvuvi na umwaguliaji, Wataalamu wa Bonde la Kati na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamezindua zoezi la uthamini wa mali za wananchi wa vijiji viwili vya Mombose na Bubutole watakaohama kupisha mradi mkubwa wa Ujenzi wa bwawa la Farkwa mkoani hapa.
Mradi wa bwawa la Farkwa ni mradi mkubwa ambao huenda ukawa ni mkubwa katika Ujenzi wa mabwawa makubwa kuliko yote barani Afrika. Mradi huu uliasisiwa na baba wa Taifa tangu mwaka 1970 utazinufaisha Wilaya za Bahi, Chemba, Chamwino na Dodoma Manispaa na utegemea kutumia pesa za Tanzania zaidi ya Tilioni 2.
Kufuatia umuhimu wa mradi huu na uwijio wa makao makuu ya nchi mkoani Dodoma, serikali imezamilia ifikapo mei mwaka huu zoezi la Uthamini wa mali za wananchi wanaohama kupisha mradi huu mkubwa katika Vijijini vya Mombose na Bubutole vilivyopo Wilayani Chemba pamoja na vijiji vinavyopitiwa na njia Kuu ya bomba linalopeleka Maji eneo la Kilimani mjini Dodoma liwe limekamilika tayari kwa kuwalipa wananchi ili Ujenzi wa bwawa uanze.
Ujenzi wa mradi huu unategemea kuchukua miaka mitatu 2017-2021 mpaka kukamilika kwake. Hivyo wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Wataalamu wa uthamini kwa kuwa wameusubiri mradi huu kwa zaidi ya miaka 47 na leo serikali imepata fedha ya kuutekeleza.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Odunga wamewataka wananchi hao kujiepusha na watu wasiopenda maendeleo yao na nchi yetu kwa ujumla wa anaopita pita huko na kujifanya watetezi wa haki za wananchi. Swali hao watetezi walikuwa wapi tangu 1970 waje leo ambapo mradi unaanza kutekelezwa.?
Aidha, amesisitiza wananchi ambao ni wamiliki halali wa maeneo husika ndio wajitokeze kwenye uthamini huo ili kuepusha udanganyifu na migogoro isiyo ya lazima wakati wa malipo yatakopoanza. Kwani kuna baadhi ya wananchi zi waaminifu na atakayefanya hivyo akibaini sheria kali dhidi yake zitachukua mkondo.
Kwa upande wa Wataalamu Mkuu huyo wa Wilaya amewataka kutumia akili, uweledi na taaluma zao katika kuhakikisha kila mwananchi wa maeneo hayo anapata haki yake stahiki kwa mujibu wa sheria za uthamini.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mhe Rajabu Muheshimwa ameongea kwa kupongeza juhudi za Serikali kwa kuamua kuanza mradi huu na zaidi kusihi wananchi kutoa ushirikiano kwa Wataalamu, hali kadhalika Mhe Diwani wa Kata ya Farkwa Ndugu, Suleiman Gawa amesisitiza kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu pia Wataalamu wahakikishe wanaorodhesha mali zote za wananchi zinazotambulika kisheria ili kuepusha migongano hapo baadae.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya amewataka Viongozi wa Vijiji na vitongoji kusimamia zoezi hili kikamilifu kwani wao ndio wanaowafahamu wananchi wao pia watoto ambao wanamiliki mali lakini hawatambuliwi kisheria kutokana na umri wao.

MAKONDA AHOJIWA NA KAMATI YA BUNGE YA HAKI,KINGA NA MADARAKA YA BUNGE HII LEO
Wednesday, March 29, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, <Maadili na Madaraka ya Bunge ambapo ilimwita kumhoji kisha ajibu tuhuma mbalimbali zinazo mkabili kiongozi huyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Simbachawene akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichoketi hii leo mjini Dodoma kumhoji Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kufuatia tuhuma mbalimbali zilizokuwa zimewasilishwa na wabunge katika Bunge lililopita.
Tuesday, 28 March 2017
WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI WA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AHADI, ILANI YA CHAMA TAWALA NA MAAGIZO YA VIONGOZI WAKUU
Tuesday, March 28, 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza
umuhimu wa mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi,
Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu wakati wa uzinduzi wa mfumo
huo Machi 28, 2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma na
kulia kwake waliokaa ni Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.

Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasilisha
hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia
Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu Ukumbi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Agustino Tendwa akiratibu shughuli ya uzinduzi wa mfumo
wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na
Maagizo ya Viongozi Wakuu uliofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Machi 28,
2017.

Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli
za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa
Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe
wa mkutano huo (hawapo pichani) Dodoma.

Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli
za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa
Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe
wa mkutano wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 Dodoma.
*****************
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amezindua mfumo mpya wa Kielektroniki wa
Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi
Wakuu ulianzishwa kwa lengo la kusaidia upatikanaji na utoaji wa taarifa za
utekelezaji kupitia mfumo wa kisasa (kidigitali).
Akizindua mfumo huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
Machi 28, 2017 Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu
wa mfumo huo kuwa umejikita katika
kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za utekelezaji wa Maagizo yao na yale yaliyoelekezwa
katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.
“Mfumo huu utasaidia sana katika kufuatilia shughuli za
Serikali ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa maazigo yote na ahadi zilizotolewa
ili kuona utekelezaji wake kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema
Mhe.Waziri.
Aidha mfumo utasaidia pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza
ufanisi wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kila siku za Serikali kwakuwa
taarifa zote zitapatikana kwa wakati na takwimu za uhakika.
Alibainisha kuwa, kuanzishwa kwa mfumo ni moja ya sehemu ya
kuondoa changamoto kadhaa ikiwa ni kuongeza ufanisi maeneo yetu ya kazi “kuanzishwa
kwa mfumo huo kutatua changamoto za uchelewashwaji wa taarifa, na kutowajibika
kwa ujumla na kuleta ufanisi kazini”.Alisisitiza waziri.
Aidha kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.
Hamisi Mwinyimvua alibainisha kuwa mfumo umepitia hatua zote muhimu ikiwa ni
pamoja na kuwashirikisha Mawaziri wote,
Makatibu Wakuu wote, Wasaidizi wa Mhe.Rais Jonh Magufuli na Watendaji wa Serikali.
Kwa kumalizia Waziri alipongeza
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao kwa kuona
umuhimu wa kuwepo kwa mfumo huu na kutoa rai kwa Watendaji wote wa Serikali kuutendea
haki kwa kufanya kazi bila uzembe wowote. “rai yangu kwa Watumishi wa
Umma wote Nchini kuwajibika kwa kufanya kazi kwani kupitia Mfumo huu, mzembe
atajulikana na mchapa kazi atajulikana. Na ikumbukwe tu, wazembe na wavivu
hawana nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano”.
MAELEZO YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. PHILIP MPANGO AKIWASILISHA MAPENDEKEZO YA SERIKALI YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA YA KIWANGO NA UKOMO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18
Tuesday, March 28, 2017
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 mbeye ya Wabunge mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akiongoza Kikao cha Wabunge wote mjini Dodoma ambacho kilipokea Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na
Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 mbeye ya
Wabunge mjini Dodoma leo.Kuhoto ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na kulia ni Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa maelezo kabla Waziri wa Fedha na Mipango haja wasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na
Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 mbeye ya
Wabunge mjini Dodoma leo.Katikati ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa anaongoza na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
Wabunge wakisalimiana kabla ya kuanza kikao.
Wabunge wakisikiliza maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (hayupo pichani) wakati Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na
Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 mbeye ya
Wabunge mjini Dodoma leo.
*************
MAELEZO
YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB)
AKIWASILISHA MAPENDEKEZO YA SERIKALI YA MPANGO
WA
MAENDELEO WA TAIFA NA YA KIWANGO NA UKOMO WA BAJETI
YA SERIKALI
KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18
Subscribe to:
Posts (Atom)