Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama amewaambia waandishi wa Habari
Mjini Dodoma leo baada ya kumaliza kikao hicho kuwa, Kamati yake imepokea
ripoti ya utendaji wa TCAA lakini wameshindwa
kuijadili baada ya kubaini kuwa watendaji wakuu wote wa mamlaka hiyo hawapo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PIC, Albert Obama akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Lolencia Bukwimba na Katibu wa Kamati hiyo wakiendelea na kikao mjini Dodoma leo.
KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa
Mitaji ya Umma (PIC) imegoma kujadili taarifa ya Malaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) hadi pale Msajili wa Hazina atakapo hakikisha kuwa Mamlaka hiyo inapata Bodi.
Mwenyekiti wa Kamati wa
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama amewaambia waandishi wa Habari
Mjini Dodoma leo baada ya kumaliza kikao hicho kuwa, Kamati yake imepokea
ripoti ya utendaji wa TCAA lakini wameshindwa
kuijadili baada ya kubaini kuwa watendaji wakuu wote wa mamlaka hiyo hawapo.
Obama alisema kuwa TCAA
wametumwa wawakilishi tu, lakini kuanzia Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi wa
Mamlaka ambao kimsingi ndio watendaji na ambao wanaidhinisha miradi hawapo.
“Kama Mkurugenzi wa TCAA
na Mwenyekiti wa Bodi hakuweza kufika basi walau tungekuwa na hata na Katibu
Mkuu basi wa Wizara,” alisema Obama.
Alisema Kamati imemwagiza
Msajili wa Hazina kwenda kuhakikisha uongozi wa Bodi na Menejimenti unakamilika
ndipo wataomba kwa Spika wapangiwe kujieleza.
Kutokana na kushindikana
kujieleza Kamati imeahirisha kuwapa nafasi kujieleza wajumbe watatu waliokuwapo
ambao nao wana kaimu nafasi zao.
“Kamati hii ni mtambuka hivyo
bila kuwapo waidhinishaji miradi na watekelezaji, ni vigumu kutoa maagizo kwa
wajumbe badala ya viongozi,”alisema Obama.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment