Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 20 January 2017

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI SITA ALIOWATEUA KWENDA NCHI MBALIMBALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Emanuel Nchimbi kuwa Balozi Nchini Brazili, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. James Msekela  kuwa Balozi Geneva –Umoja wa Mataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mbelwa Kairuki kuwa Balozi nchini China, Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha George Madafa kuwa Balozi nchini Italia
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Elizabeth Kiondo kuwa Balozi nchini Uturuki
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Fatma Rajab  kuwa balozi nchini Qatar, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi wateule wakila kiapo cha Uadilifu mara baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Balozi Emanuel Nchimbi, Balozi Dkt. James Msekela  ,Balozi Mbelwa Kairuki, Balozi George Madafa, Balozi Prof. Elizabeth Kiondo na Balozi Fatma Rajab  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Mabalozi wateule mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi mbalimbali aliowaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
******************
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo Januari 20, 2017 amewaapisha Mabalozi sita aliowateua jana kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mabalozi walioapishwa ni Dkt. Emmanuel John Nchimbi - Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dkt. James Alex Msekela - Balozi wa Tanzania Geneva - Umoja wa  Mataifa,  Mbelwa Brighton Kairuki - Balozi wa Tanzania nchini China, 

Fatma Mohamed Rajab - Balozi wa Tanzania nchini Qatar, George Kahema Madafa - Balozi wa Tanzania nchini Italy,  Prof. Elizabeth Kiango Kiondo – Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Wakati huo huo, Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Reginald Nsekela amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Rais  Dkt. John Pombe Magufuli.

Baada ya kula kiapo cha Uadilifu,  Jaji Mstaafu Nsekela ameongoza kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kwa Mabalozi sita walioapishwa leo kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

Akizungumza baada ya Mabalozi hao kula viapo vyao, Rais Magufuli amewataka kuiwakilisha vizuri Tanzania katika nchi walizopangiwa kwa kuhakikisha wanasimamia maslai ya Tanzania.

“Nendeni mkatekeleze kazi zenu kwa upendo mkubwa mkijua umma wa Watanzania upo nyuma yenu, Maslai ya Watanzania yakawe mbele, Tanzania kwanza ikawe mbele, na mimi nina uhakika mtakuwa mmewafanyia Watanzania mema na mazuri sana”  “Ukiona kizuri chochote kwa ajili ya Watanzania kilete, mkatetee Tanzania, mkajenge


uchumi wa Tanzania, mkaimarishe mahusiano ya Tanzania, mkajenge urafiki wa Watanzania, mkajenge biashara za Watanzania” amesema Rais Magufuli. 


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment