Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 17 January 2017

POLISI MBEYA WAZUNGUMZIA TUKIO LA MAITI YA MTOTO ILIYOKUTWA NDANI BAADA YA MAZIKO

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ,Dhahiri Kidavashari.
Wakazi wa Isanga Jijini Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya tukio lisilo la kawaida ambapo maiti iliyokwenda kuzikwa katika makaburi ya zamani ya Isanga ilikutwa ikiwa kwenye godoro ndani ya nyumba alimofia.

Taarifa yaJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya inasema kuwa mnamo tarehe 16.01.2017 majira ya saa 4:30 asubuhi katika mtaa wa Igoma “A”, Kata ya Isanga, Jijini Mbeya.

Kufuatia taarifa hiyo Polisi walifuatilia na kubaini kuwa tarehe 16.01.2017 majira ya saa 1:00 asubuhi mtu mmoja aitwaye JAILO KYANDO na mke wake aitwaye ANNA ELIEZA wote wakazi wa mtaa wa Igoma “A” waliamka asubuhi na kukuta mtoto wao wa kwanza aitwaye HARUN JAILO KYANDO amefariki dunia akiwa amelala.

Taarifa za awali zinadai kuwa marehemu tangu utoto wake alikuwa na matatizo ya ugonjwa wa kifafa hali iliyopelekea kuishi nyumbani pasipo kusoma.

Kufuatia kifo hicho msiba uliendeshwa na taratibu za mazishi zilifanyika. Majira ya saa 6:00 mchana jeneza lililetwa msibani na kuwekwa sebuleni kando ya mwili wa marehemu ambao ulikuwa umeviringishwa na blanketi na kulazwa chini kwenye godoro, baada ya maombi yaliyoongozwa na walokole waitwao BONDE LA BARAKA vijana walibeba jeneza hadi makaburi ya zamani ya Isanga na kisha jeneza kuzikwa.

Waombolezaji waliporudi nyumbani walitaharuki kuona mwili wa marehemu mtoto HARUN JAILO KYANDO ukiwa chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali. Kutokana na hali hiyo taarifa zilifikishwa Polisi mara moja, askari Polisi walifika na kurejesha hali ya amani kwa kuuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Taratibu nyingine za mazishi zitafanyika leo tarehe 17.01.2017. Mpaka sasa bado haijafahamika ni uzembe /bahati mbaya wafiwa kusahau kuweka mwili wa marehemu kwenye jeneza au kulikuwa na hujuma zozote. Upelelezi unaendelea kuhusiana na tukio hili.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment