Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu
Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu
Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School kushoto ni Meneja Mradi Dkt Charles Sokile.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania uliomtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameuhimiza uongozi wa Taasisi ya Kingdom
Leadership Network Tanzania(KLNT) kuharakisha mchakato wa kuanzisha kituo
cha Joseph Business Centre(JBC) kwa ajili ya maboresho ya uchumi wa nchi na
ukuzaji viwanda.
Moja kati ya malengo ya chuo hicho ni
kusaidia na kuhimiza maendeleo ya viwanda na kupitia ugundunzi ya mawazo ya
biashara na viwandani (Incubation Centre) ya Sayansi, Teknolojia, Kilimo cha
biashara, uzalishaji na utalii.
Makamu wa Rais ametoa kauli ofisini
kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo alipokutana na kufanya mazungumzo na
Viongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania(KLNT) ambao
walimtembelea Makamu wa Rais kumweleza hatua ambazo wamefikia katika uanzishaji
wa kituo na Chuo hicho.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
amesema wazo la uanzishaji wa Kituo na Chuo hicho ulitolewa na Dkt Bill Winston
ambaye ni Mwanzilishi wa Chuo cha Joseph Business School, Chicago nchini
Marekani na Bill Winston Ministries mwaka jana katika Maombezi ya Taifa(
National Prayer Breakfast) ambaye yeye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo,
anasema aliupokea kwa furaha mpango huo kwa sababu kituo na chuo hicho
kitasaidia watanzania wengi kupata elimu na ujuzi wa kuimarisha biashara zao
wakati taifa likielekea kwenye uchumi wa Viwanda.
Amesema hatua za uanzishwaji wa kituo
na Chuo hicho hapa nchini ni fursa pekee na nzuri kwa Watanzania kujifunza
ubunifu na ugunduzi katika biashara, maadili ya uongozi katika biashara ili
kuongeza ufanisi katika biashara zao kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa
ujumla hasa katika ulipaji wa kodi.
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa bodi
Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma, Mkurugenzi wa
Mradi wa JBC Dkt Charles Sokile wamemhakikishia Makamu wa Rais kuwa hatua
ambazo wamefikia kwa sasa katika uanzishaji wa kituo na Chuo hicho ni nzuri
ambapo mpaka sasa wamepata majengo kwa ajili ya ofisi na maeneo ya kufundishia
na hatua za usajili wa chuo hicho zipo katika hatua za mwisho.
Watendaji wa KLNT wamesisitiza kuwa wanataka
kushirikiana ipasavyo na Serikali katika uanzishaji wa kituo na chuo hicho
ambacho kitatoa elimu ya biashara hasa ugunduzi wa mawazo ya biashara nchini
kama hatua ya kutekeleza kwa vitendo dhana ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda
nchini.
Taasisi ya KNLT ni taasisi
ya kizalendo, ambayo inashugulikia maswala ya uadilifu kwenye uongozi, uchumi,
uwekezaji na katika biashara imekuwa ikifanya shughuli zake hapa nchini kwa
faida na tija ya maendeleo ya taifa.
Katika kituo hicho cha JBC kutakuwa
kitengo cha kusaidia fedha za mitaji kwa wahitimu waliofanikiwa kulelewa mawazo
ya kibiashara yenye tija kwa Taifa, na mahusiano ya kibiashara kati
ya Tanzania na Marekani.
Kulingana na maelezo ya watendaji hao
tawi la Chuo cha Joseph Business School (JBS) hapa nchini
chini ya chuo cha Kingdom Leadership Institute(KLI) ambacho kitatoa
mafunzo mbalimbali ya biashara, maadili ya uongozi na ugunduzi wa mawazo ya
biashara ili kusaidia mamia ya Watanzania kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment