Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo.
Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2015/16.
Ukusanyaji wa mapato katika
kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74.
Mlinganisho wa makusanyo ya mapato
kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
MWEZI
|
MWAKA
2015/16
|
MWAKA
2016/17
|
Ongezeko
|
JULAI
|
925,384.7
|
1,069,458.5
|
15.57
|
AGOSTI
|
923,316.9
|
1,154.222.5
|
25.01
|
SEPTEMBA
|
1,132,310.3
|
1,378,048.9
|
21.70
|
OKTOBA
|
1,037,179.8
|
1,131,094.9
|
9.05
|
NOVEMBA
|
1,027,
939.6
|
1,123,509.7
|
9.30
|
DISEMBA
|
1,403,
189.8
|
1,414,921.8
|
0.84
|
JUMLA
|
6,449,321.1
|
7,271,256.26
|
12.74
|
Jitihada mbalimbali
zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika
ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya
ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba
mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine
za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.
TRA inaendelea kuhimiza wafanyabiashara
wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT
kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha
ya 2016.
Pamoja na hayo tunawakumbusha
na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za
Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31
Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.
TRA inatoa wito kwa
wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate
mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
Kwa wafanyabiashara wenye
madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya
kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.
Wamiliki wa majengo wanaaswa
kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari .
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI
WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment