Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe aliyoizindua leo
(hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa
Bodi hiyo iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Mwenyekiti
wa Bodi Hospitali ya Mirembe, Prof. Gadi Kilonzo akiongea na Wajumbe wa
Bodi ya Hospitali hiyo (hawapo pichani) pamoja na
wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika
Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.Mwenyekiti
wa Bodi Hospitali ya Mirembe, Prof. Gadi Kilonzo akiongea na Wajumbe wa
Bodi ya Hospitali hiyo (hawapo pichani) pamoja na
wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika
Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Mganga
Mkuu na Katibu wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe, Erasmus Mndeme akiongea
na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe pamoja na
wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika
Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi. Doroth Gwajima akiongea na Wajumbe wa Bodi leo (hawapo pichani) pamoja na
wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika
Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiwakabidhi vitendea kazi baadhi ya Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo
wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika
Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Baadhi
ya Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe pamoja na wageni wengine
waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi leo 08/02/2017 mkoani
Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika
Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Hospitali ya Mirembe baada ya hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Hospitali ya Mirembe baada ya hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Hospitali ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
*****************************
NA Benedict Liwenga-WHUSM
SERIKALI imesema kwamba tatizo la maradhi yasiyoambukiza
yakiwemo magonjwa ya akili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku huku vyanzo
vyake vikiwa ni pamoja na urithi, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe,
matatizo ya kisaikolojia pamoja na hali ngumu ya maisha.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokuwa
akizindua Bodi ya Hospitali ya Mrembe Mkoani hapo.
Akiongea na mbele ya Watendaji wa Bodi hiyo, wageni waalikwa
pamoja na Viongozi wa hospitalini hapo, Waziri Ummy amesema kuwa, kundi
lililoathirika Zaidi na kdhai hiyo ni vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa,
ambapo alitaja taarifa ya Shirikala Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2016n
inayoonyesha takribani watu milioni 15.3 Duniani wanapata matatizo ya kiafya
yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya pombe kupita
kiasi.
“Matatizo haya yamekuwa yakisababisha vifo milioni 3.3 kila
mwaka Duniani kote, hata hivyo taarifa ya Wizata yangu inaonyesha kwamba idadi
ya watu wanaougua magonjwa ya akili inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa
136,710 mwaka 2011/2012 hadi wagonjwa 448,997 mwaka 2015/2016”, alisema Ummy.
Ameongeza kuwa, takwimu za hospitali ya Mirembe zinaonyesha
kuwa, katika kipindi cha miaka mine kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, jumla ya
wagonjwa Zaidi ya 60,000 wenye magonjwa ya akili na waathirika wa dawa za
kulevya walipatiwa huduma za afya na utengamao.
Aidha, kwa kutambua majukumu makubwa ya hospitali hiyo na
kutatua changamoto zinazohusiana na magonjwa hayo, Serikali imeamua kuunda Bodi
ya hospitalini hapo lengo likiwa ni kutekeleza dhana ya Utawala Bora na Utoaji
wa Huduma Bora za Afya ya Akili kwa mujibu wa mapango mkakati na sera za nchi.
“Ninayo furaja leo kushiriki nanyi katika uzinduzi wa Bodi
hii ya Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, na bodi hii itaongozwa na Mwenyekiti
pamoja na Wajumbe walioteuliwa kutoka maeneo mbaimbali ya kiujuzi hapa
nchini”, alisema Waziri Ummy.
Amesema kuwa, bodi hiyo itakuwa na majukumu mbalimbali
yakiwemo kusimamia utendaji wa hospitali hiyo na Taasisi ya Isanga, kuhakikisha
kuwa Sheria ya uanzishwaji wa hospitali inapatikana kwa wakati, kushauri kuhusu
muundo wa hospitali, kuunda kamati ndogo ndogo, kushauri kuhusu mpango wa muda
mrefu ili kuboresha huduma pamoja na kushauri jinsi ya kupunguza gharama za
uendeshaji hospitalini hapo.
Sambamba na kuzindua bodi hiyo, Waziri Ummy ameitaka jamii
kushirikiana na Serikali katika kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya
hususan kwa vijana ili nguvu kazi ya Taifa isizidi kupotea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Gadi Kilonzo
amempongeza Waziri Ummy na kwa kuzindua bodi hiyo na amemuhakikishia kuwa bodi
hiyo itatekeleza maagizo yote pamoja na majukumu iliyopewa ili kuboresha
utendaji kazi hospitakini hapo.
“Dhama uliyotupa sisi Wajumbe wa Bodi ni kubwa, tunaieheshimu
sana na pia nakuahidi kuwa, tutatekeleza kwa bidii majukumu yote ya kuisimamia
hospitali hii, tutajitahidi kwa uwezo wetu wote kutatua changamoto za hospitali
hii kwa kushirikiana na wadau wengine wa afya kupitia Wizara yako, pia
tunashukuru kwa vifaa vya kazi ulivyotupatia kwa ajili ya kutumia wakati wa
utendaji wetu”, alisem Kilonzo.
Wajumbe waliochaguliwa kuunda bodi hiyo ni Profesa Gadi
Kilonzo ambaye ndio Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Erasmus Mndeme ambaye ni
Katibu wa Bodi na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mirembe, Dkt. Mpona Boniventura
ambaye ni Mwakilishi kutoka chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Joseph Mbatia, Ndugu
John Sipendi, Ndugu Ernest Kabohola, Ndugu Jane Magembe pamoja na Ndugu Clavery
Lyela.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment