Katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, Ubalozi wa Marekani na
Kituo cha Kijinsia cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo waliandaa
mdahalo wenye dhima: “Usimuache Mwanamke Nyuma” ambapo zaidi ya wanawake
300 walihudhuria mdahalo huo
katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kaimu Balozi wa
Marekani, Dk. Inmi Patterson, na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, Dk. Bonaventure Rutinwa, walitoa hotuba za ufunguzi
wakati wanawake maarufu wa Kitanzania walishiriki
katika mdahalo, wakiwemo Vicky Ntetema, Mwanaharakati wa haki za
kibinadamu, Joyce Mhaville, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Dk.
Victoria Kisyombe, Mwanzilishi wa taasisi ya Selfina, Profesa Costancia
Rugumamu, mtaalamu wa masuala ya kijinsia na maendeleo
Chuo Kikuu cha Dar es Salaama, na Abella Bateyunga, mwanzilishi wa
Tanzania Bora Initiatives, ambaye alikuwa mwezeshaji wa mdahalo. (Picha
kwa Hisani ya Ubalozi wa Marekani).
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment