Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Chief wa kihehe Evaristo Sambiligunga Mwambeta alipokutana na machief wa kihehe kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kulia) akizungumza na Machief wa kihehe (hawapo pichani) alipokutana nao kuzungumzia namna ya kuhifadhi historia ya ukombozi wa Bara
la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(wapili kulia) katika picha ya pamoja na machief wa kihehe baada ya kuzungumza
nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa
Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(watatu kushoto) akiwasili katika makumbusho ya Mtwa Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa
ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na kuendeleza historia ya
shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa harakati za kuwakomboa
wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani Iringa. Watatu kulia ni
Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi
Mduma
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(wapili kushoto) akiangalia fuvu la Mtwa Mkwawa alipotembelea makumbusho ya
Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na
kuendeleza historia ya shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa
harakati za kuwakomboa wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani
Iringa.
Mtaalamu kutoka makumbusho Mkwawa
(kulia) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrion
Mwakyembe (wapili kulia) baadhi ya vifaa alivyotumia Mtwa Mkwawa wakati wa
harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika
makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(katikati) akiwa ameshika silaha za jadi alizokuwa anatumia Mtwa Mkwawa wakati
wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika
makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(katikati) akiangalia kaburi la Mtwa Abdul Adam Sapi Mkwawa alipotembelea
makaburi ya machief kutoka ukoo wa Mkwawa jana katika makumbusho ya Mkwawa
iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano iliyopo katika
mnara wa Frelimo alipotembelea mnara wa Frelimo uliojengea na serikali ya
Tanzania mwaka 1977 kwa lengo la kutoa heshima na kumbukumbu kwa aliyekuwa
kiongozi wa chama cha ukombozi nchini Mozambiki Bw. Samora Machel.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Msingi Muungano akijibu swali la kihistoria
lililoulizwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe wakati wa ziara yake katika mnara wa Frelimo ulipo katika shule ya
Muungano jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(watatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Halmashauri ya
Iringa katika mnara wa Frelimo uliojengea na serikali ya Tanzania mwaka 1977
kwa lengo la kutoa heshima na kumbukumbu kwa aliyekuwa kiongozi wa chama cha ukombozi
nchini Mozambiki Bw. Samora Machel.
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Gibson Sanga (kushoto) akimuonyesha
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(katikati) baadhi ya vifaa vya kitamaduni vinavyotumiwa na kabila la wahehe
alipotembelea makumbusho ya Iringa jana Mkoani Iringa. Picha
na:
Genofeva Matemu - WHUSM
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment