Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Kangi Lugola
akisalimiana na Dotto Roman Selasini
Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Iramba mara baada ya kuwasili katika Mgodi
wa Senkenke One ulipo katika Kijiji cha Nkonkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya
Shelui, Wilaya ya Iramba akiongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,
Biashara na Mazingira kutembelea mgodi huo kwa lengo la kujionea hali ya
mazingira mgodini hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Kangi Lugola (katikati)
akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira, Murad SadickA (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel
Lwehaula wakati wa ziara ya kutembelea mgodi wa Sekenke one Mkoani Singida.
Wabunge wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,
Biashara na Mazingira wakiangalia zoezi la uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia
zebaki mara baada ya kutembelea mgodi wa Sekenke one Mkoani Singida.
Wachimbaji wadogo wadogo wa Sekenke one wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Kangi Lugola (hayupo pichani) alipopata fursa ya kuzungumza nao na kusisitiza suala la usafi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Kangi Lugola akifafanua
vifungu vya Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kwa watendaji wa Wilaya ya Iramba
na kuwataka kuisimamia ili kudhibiti vitendo vya uchafuzi wa Mazingira.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment