Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 26 October 2017

NDEGE NDOGO YA COASTAL AIR AMEPATA AJALI SERENGETI.

ABIRIA wawili kati ya 10 na rubani wa ndege ndogo mali ya Kampuni ya Coastal Aviation wamejeruhiwa baada ya ndege waliokuwa wakisafiria kupata ajali katika Hifadhi ya Serengeti  jana Oktoba 25,2017.

Taarifa za awali zinaarifu kuwa ndege hiyo aina ya Cessna Grand Caravan iliyokuwa imebeba abiria 10 na rubani mmoja ilipata ajali katika uwanja mdogo wa Lobo uliopo katika hifadhi ya Serengeti wakati ikijaribu kutua majira ya Saa 8:30mchana.

Abiria wawili na rubani wa ndege hiyo walipata majeraha madogo na kukimbizwa kwa matibabu jijini Nairobi wakisindikizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Juliana Edmunds.

Ndege hiyo inadaiwa iligonga mawe kisha mti na kuharibika vibaya wakati wa ajali hiyo.

Mamlaka husika zimearifiwa kuhusiana na ajali hiyo na Kampuni ya Usafiri wa Anga ya Coastal imeahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika wakati uchunguzi wa ajali hiyo ukifanyika.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment