Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 30 August 2017

WABUNGE WAHOJI UBINASHISHAJI VIWANJA VYA NDEGE

UBINAFSISHAJI wa Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege (KADCO), umehojiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa umegubikwa na utata, hali ambayo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wametaka wapewe maelezo ya serikali, vinginevyo suala hilo litahamishiwa bungeni lijadiliwe.

Hayo yalibainika jana katika kikao kati ya wajumbe wa PAC na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Miongoni mwa mambo ambayo wajumbe walisema yana utata, ni pamoja na CAG kubaini kuwa licha ya serikali kuwa na hisa asilimia 100 katika Kadco, kampuni hiyo imeendelea kuachiwa kuendesha Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KIA).

Utata mwingine ni hatua ya KIA kuendeshwa tofauti na viwanja vingine, kwa maana ya kuwa chini ya kampuni hiyo wakati viwanja vya ndege vingine vyote viko chini ya TAA. "Kwa nini hiki kiendeshwe tofauti na viwanja vingine?
 BOFYA HAPA KUOSOMA ZAIDI.
 Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ikiwa katika kikao chake Mjini Dodoma jana. Picha na Mroki Mroki-Daily News Digital.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa TAA.
 Mmoja wa maofisa wa TAA akitoa ufafanuzi wa baadhi ya vitu.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Prof. Ninatubu Lema, akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ikihoji TAA.
 Watendaji wa TAA wakisikiliza hoja za Kamati.
Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao chao mjini Dodoma.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment