Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.
RAIS Dkt.
John Magufuli, yupo mkoani Mwanza kwa ziara
ya kikazi ya siku mbili.
Rais Magufuli aliwasili jana Julai 3 mwaka huu jijini Mwanzan na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongela pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza.
Akiwa mkoani humo, Rais Magufuli atakuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji
wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Sengerema utakaofanyika leo Julai 4,
2017.
Katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Rais Dkt.
Magufuli aalikutana na kamati ya amani ya viongozi wa dini na kuwashukuru viongozi hao kwa sala na dua zao
na amewataka waendelee kuwahimiza waumini wao kuliombea Taifa ili liepukane na
vitendo vya rushwa ambavyo ni adui wa maendeleo.
Akiwa njiani kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza
katika eneo la Bwiru kuelekea Ikulu ndogo ya Mwanza, Rais Magufuli msafara
wake umesimamishwa mara kwa mara na wananchi waliojaa barabarani na kuamua kuzungumza
nao ambapo amewahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imepania kupambana na
ufisadi kwa lengo la kuwaletea maendeleo Watanzania bila kujali tofauti za dini
au Siasa.
Aidha, amewahakikishia wananchi hao kuwa
Serikali yake imedhamiria kuondoa kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufuta
baadhi ya kodi zenye kero na kuwapatia vitambulisho wafanyabishara wadogo
wadogo, maarufu kama Wamachinga, ili waweze kufanya biashara zao bila
kusumbuliwa.
Akiwa eneo la Nyamagana jijini Mwanza,
Rais alitembea kwa miguu huku kuwasalimu wananchi waliokuwa
wakimshangilia na kuzuia msafara wake. Rais Magufuli pia alikwenda Uwanja wa Mpira wa Nyamagana na kuungana na
baadhi ya wananchi waliokuwa wakiangalia mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Buhongwe na Nyamwaga.
Rais Dkt. Magufuli pia amefurahishwa na
maendeleo ya ujenzi wa barabara ya kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi
katikakati ya jiji ambao gharama za ujenzi wake zilitokana na fedha zilizokuwa
zimetengwa kwa ajili ya sherehe za Muungano.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment