Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali maombi ya upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Jamal Malinzi na wenzake ya kuomba dhamana.
Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya utakatishaji fedha ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na mweka hazina, Nsandie Mwanga.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema, hata upande wa utetezi unajua kuwa mashitaka ya utakatishaji fedha hayana dhamana.
"Suala la kujiuliza, je mahakama hii inamamlaka ya kutoa dhamana katika kesi ya utakatishaji fedha?. Tunaona kuwa upande wa utetezi kupitia wakili Jerome Msemwa hawakubisha kama makosa hayo hayana dhamana," amesema Hakimu Mashauri
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kwa sababu upelelezi haujakamilika
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment