NUKUU MBALIMBALI ZA RAIS DK JOHN MAGUFULI WAKATI WA AZKIZUNGUMZA HII LEO KATIKA UZINDUZI WA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM.
****************
#"Inaonekana kina mama
wanaosimamia mashirika ya maendeleo wanafanya kazi nzuri, hata huu mradi ambao
umegharimu zaidi ya bilion 900 umewezeshwa na wao," Rais John Magufuli
#"Ufanisi na utendaji
mzuri wa reli ya standard gauge utategemea ufanisi wa bandari hii, hivyo mtaona
ni jinsi gani ni muhinu. Upanuzi huu utaongeza shehena ya mizigo na hivyo
kuwezesha serikali kukusanya mapato,"
Rais John Magufuli
#"Unatarajiwa kukamilika
kwa miezi 36 kama mkataba unavyosema, lakini,nataka miezi 30 iwe imekamilika
lakini ikiwezekana hata miezi 28, fedha zipo sasa wakae miezi 36 hapa wanafanya
nini," Rais John Magufuli
#"Ilitakiwa hii bandari iltakiwa iwe imepanuliwa zamani, wafanyabiashara walikuwa wanalamimika bila kusema
sababu, tulikuwa na eneo ambalo halitoshi labda ulete mitumbwi na viboti hivi.
Tulikuwa tunasema tuna bandari lakini kumbe upande mmoja ni bandari na upande
mwingine ni mwalo," Rais John Magufuli
#"Ikishakamilika bandari
hii itakuwa ni ya mfano kwa sababu zitakuwa meli nyingi zinakuja kwa wakati
mmoja, kutakuwa hakuna ucheleweshaji labda kama TPA wacheleweshe kwa makusudi
na hao watakaochelewesha ndio tutalala nao vizuri," Rais John
Magufuli
#"Pakiwa na facility nzuri
hapa tutakuwa tunapromote uchumi wa nchi zingine. Bahati nzuri sisi ni
wanachama wa SADC na EAC... hivyo watu kama milioni 500 watanufaika na bandari
hii," Rais John Magufuli.
#"Serikali ya wamu ya tano imedhamiria kuboresha miundombinu ya usafiri na kudhihirisha hilo,
tunaendelea na upanuzi wa bandari mbalimbali, viwanja vya ndege na
barabara," Rais John Magufuli
#"Bandari mmeanza vizuri
lakini nataka kwenye hizi ICDs, hizi ziliwekwa kwa ajili mizigo ikijaa hapa
ndio ipelekwe kule lakini sasa hivi inapelekwa hata kabla haijajaa na kuna
kamchezo fulani...mizigo inasemwa ni transit lakini inauzwa humu humu, kuna
kampuni fulani inafanya huo mchezo wa kukwepa kodi fuatilieni hilo," Rais
John Magufuli
#" Kuna vichwa 13 vya
treni vimeshushwa hapa lakini havijulikani ni vya nani, tena inasemekana ni
vibovu na TRL wamesema hawajaagiza na wala hwajasaini mkataba wowote.
Hamkuuliza vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku nyjngine si
watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu," Rais John
Magufuli
#"Sijui haya mavichwa
mtafayanyia nini, lakini hili nj lazima lisemwe ili Watanzania wafahamu.
Tutangulize uzalendo wa nchi yetu
#"Niwaombe wanasiasa
wanaoshindwa kucontroll midomo ya, wanaosema kuwa hawa watu wameshikwa kwa muda
mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda
nrefu, katika hali hiyk kwanini usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.
Msitufanye tukafika huko," Rais John Magufuli.
#"Kwanini hata siku moja
mtu asijitokeze kuulani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa kuta sifa za
kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu
wanakufa kule...nataka polisi mfanye kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie
polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni
ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani," Rais John Magufuli
#"Juzi mtu amekamatwa na
uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu
unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa waliogiza hizo uniform
za jeshi," Rais John Magufuli.
#"Endeleeni kujenga
heshima ya bandari, rushwa iwe ni marufuku, halafu muda pia... mtu akifika hapa
akae muda mfupi na aondoke, hata kama anasafirisha pini ifike inapokwenda na
sio ipotelee njiani," Rais John Magufuli
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment