Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 2 July 2017

KAMPUNI YA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN) KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

 MIONGONI mwa Kampuni za Kitanzania ambazo zimeshiriki Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam kwa mwaka huu ni Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji na wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Habarileo na Sportleo laikini pia yapo Sundaynews na Habarileo Jumapili.

Katika magazeti hayo kuna majarida mbalimbali yanayochapishwa kila siku lakini majarida makubwa zaidi ni ACADEMY linalowekwa kila Jumatano na ELIMIKA linalotoka kila siku ya Alhamisi na majarida haya ni maksusi kwaajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi kuanzia Shule za Msingi hadi Sekondari. Wanafunzi wa Shule za Kiingereza na zile za kawaida yanawafaa sana haya. 
 TANGAZA NASI SASA.
Wasiliana nasi kupitia namba 0755373999 au 0712516169 nasi tutaweza kufika katika Banda lako na kukupa huduma ya kutoa habari za kazi na huduma unazotoa kwa gharama nafuu kabisa kupitia Blog hii na Magazeti ya Daily News, Habarileo na Sportleo. 
 Wafanyakazi mahiri wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wapo katika banda la Maonesho la Jakaya Kikwete yanapofanyika maonesho hayo katika Viwanja vya Mwalimu Julis Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mzazi ukiingia katika mabanda hayo hakikisha unapita katika Banda la TSN ili uweze kupatiwa majarida hayo. Na ujue namna ya kuyapata kila Jumatano na Alhamisi kuweza kumsaidia mtoto wako. 

Lakini Pia Kampuni ya TSN, inatoa huduma mbalimbali zikiwepo za Matangazo katika magazeti yake na katika msimu huu wa Sikukuu inatoa opunguzo la bei hadi asilimia 20 kwa kila tangazo katika magazeti yake lakini pia kupitia Blogg hii ya TSN na mitandao mingine ya kijamii iliyonayo. 

TSN pia wanatoa huduma za Upigaji Picha katika Matukio mbalimbali ya Kimafamilia na yale ya kibiashara. Pia unaweza kuchapiwa magazeti yako, vitabu, Kalenda na vitu vingine mbalimbali.
 Wakazi wa Dar es salaam wakifurahia huduma katika Banda la Magazeti ya Serikali na kupewa zadi ya Kalenga Kubwa ya Ukutani na Majarida mbalimbali yanayochapishwa na TSN.
Mmoja wa wanachi akiuliza maswali na kuhudumiwa.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment