Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Sunday, 30 July 2017

CHUO CHA IFM CHATENGA WIKI NZIMA YA KUTOA MAELEZO NA KUFANYA UDAHILI KWA WANAOTAKA KUJIUNGA NA CHUO HICHO

 Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk. Kadida Mashaushiakizungumza na Blog ya Daily News-Habarileo juu ya Wiki moja kwa ajili ya kutoa ufafanuzi, maelekezo na kufanya udahili wa kozi mbamlimbali zinazotolewa na chuo hicho.
 Watu mbalimbali waliofika chuoni hapo kwajili ya kupata amelezo juu ya namna ya kujiunga na chuo hicho wakisikilizwa na maofisa wa chuo.
CHUO Cha Usimamizi wa Fedha nchini (IFM) kimetenga mda wa wiki moja kwa ajili ya kutoa ufafanuzi, maelekezo na kufanya udahili wa kozi mbamlimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii katika Chuo Hicho Dk. Kadida Mashaushi alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa zoezi hilo litaanza tarehe 29 mwezi huu na kumalizika tarehe 5 mwezi ujao (8) katika Chuo hicho kilichopo jijini hapa.

“Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam na wale wa mikoa ya jirani, fursa hii ambayo imetolewa na chuo cha usimamizi wa fedha nchini ni adimu kwa kutoa maelekezo kwa wazazi, wanafunzi watarajiwa, waombaji na wadau mbalimbali kuzielewa kwa usahihi kozi mbalimbali ambazo zinatolewa na chuo,” alisema.

Dk Mashaushi alisema kuwa zoezi hilo ni mwitikio wa chuo hicho baada ya serikali kutoa muongozo kwa namna ambavyo wanafunzi wapya wa elimu ya juu watadahiliwa mwaka huu wa masomo (2017/18) na maelekezo yaliotolewa kuhusu vigezo vya kuingia elimu ya juu.

Alisema kutokana na maelekezo hayo, kumekuwepo na mkanganyiko miongoni mwa wa wadau mbalimbali kwenye sekta ya elimu ya juu hususani kwa  upande wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini, hivyo kupelekea chuo hicho kuanzisha hilo zoezi kwa ajili ya kusaidia katika kutatua changamoto hizo.

“Zoezi hili litasaidia wale ambao wanatamani kuingia elimu ya juu, kuwawekea wepesi wa kutosha ili kufanikisha malengo yao,” alisema na kuongeza kuwa katika zoezi hilo, chuo hicho kinatoa maelekezo ya kina na kujibu maswali yale ambayo jamii kwa ujumla imekanganyikiwa baada ya mabadiliko ya udahili yalitolewa mwaka huu na serikali.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni uelewa usietosheleza kwa muomba na kupelekea baadhi ya wao kuomba kozi ambayo hana sifa nayo na ombi lake kwenda kwa katika kozi mabayo sio sahihi na baadaye kutochaguliwa.

Mashaushi alisema pia wakati huohuo vyuo navyo huenda viakapata wanafunzi wachache katika zile nafasi ambazo zipo. Zoezi la udahili kwa wanafunzi wa elimu ya juu linatrajiwa kusitishwa tarehe 30 mwezi ujao (8) mwaka huu.

“Changamoto kubwa kwa vyuo kutokua ufafanuzi ili kila mwenye alama zinazotosheleza akapata kuomba kwa usahihi kwa mujibu wa vigezo viliwekwa na serikali, vyuo na taratibu ambayo serikali imeweka mwak huu,” aliongeza.

Kwa hatua nyingine, Dk.Mashaushi alisema kuwa kwa wale wa mikoa ya mbali, watapata taarifa mbalimbali kuhusu udahili wa mwaka huu kupitia tovuti ya chuo ambapo pia watapata fomu ya maombi ya kujiunga na chuo.

“Kwa wale wa Mwanza watapata maelekezo, ufafanuzi katika kituo chetu cha mafunzo kilicho huko  ambapo watakutana na maaofisa wetu. Na wale wengine ambao pia hawataweza kufika wanaweza kutumia tovuti yetu na njia ya posta katika kuwasilisha fomu zao,” alisema.

IFM imejikita katika kutoa kozi za uhasibu ngazi ya shahada, stashahada na cheti. Pia chuo hicho kimejikita katika fani ya bima na hifadhi ya jamii ambapo halikadhalika inatolewa kozi ya shahada kozi ya bima na hifadhi ya jamii na kozi maeneo ya kodi kwenye ngazi ya shahada, stashahada na cheti.

“Chuo pia kiko vizuri na miongoni mwa vyuo vichache  ambavyo vinatoa mafunzo katika maswala ya bank na fedha katika ngazi ya shahada  (Bachelor of banking and finance) na stashahada (ordinary diploma in banking and finance) na cheti kwa wanafunzi watarajiwa elimu ya juu.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment