Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 30 June 2017

LYANGA ATEULIWA KUWA KAMANDA WA KANDA MAALUM YA PWANI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amemteua,  Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Onesmo Lyanga kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Pwani ikiwa ni hatua ya kupambana na matukio ya uhalifu katika maeneo ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga. Anaandika Katuma Masamba.

IGP Sirro amemtangaza Lyanga kuchukua nafasi hiyo leo (Ijumaa) katika makao makuu ya jeshi hilo wakati akizungumza na wanahabari.

“Wananchi wampe ushirikiano kwa sababu matatizo ya kule hayawezi kumalizwa na vyombo vya dola, bali kwa kushirikiano na wao, watoe taarifa ili hawa wahalifu wapatikane,” amesema Sirro.

Lyanga kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alikuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema, kwa ssaa serikali inafanya jitihada za kurekebisha miundombinu ili kanda hiyo mpya iweze kufanya kazi zake vizuri.

“Kanda hii imeshaanza kazi na Kamanda wake ameshateuliwa… suala la kumaliza uhalifu Kibiti na Mkuranga ni suala ambalo halina mjadala ni suala la lazima,” amesema.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment