Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 20 June 2017

BURIANI ALLY YANGA

SIMANZI imetawala miongoni mwa mashabiki wa mpira wa miguu nchini Tanzania, hususani wapenzi na mashabiki wa timi ya Yanga yenye maskani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo cha shabiki wake na mnazi wa timu hiyo, Allya Yanga. Anaandika Mroki Mroki.

Ally Yanga aliyejizolea umaarufu nchini alifikwa na umauti hii leo kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea leo  mchana mkoani Dodoma akiwa katika shughuli zake za kikazi.
Ajali iliyotwaa uhai wa Ally, inaarifiwa kutokea kijiji cha Chipogolo kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma njia ya kwenda mkoani Iringa kilichosababishwa na ajali ya gari iliyokuwa ikimkwepa mwendesha bodaboda aliyeingia barabara kuu bila tahadhari.
Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipinduka na kumrushanje Ally Yanga ambaye anadhaniwa kuwa hakuwa amefunga mkanda na kuwaacha webnzake waliokuwa gari moja wakiwa majeruhi.

Blog hii ya DAILY NEWS-HABARILEO inatoa pole kwa ndugu, jamaa na familia yote ya marehemu kufuatia msiba huo mzito. 
 Ally Yanga akiwa katika suti na tai, wakatri Yanga ikicheza mechi za Kimataifa nyumbani.
 Shabiki wa Yanga, Ally Yanga akiwa jukwaani katika sura tofauti tofauti enzi za uhai wake hasa pale alipokuwa akiona matokeo si ya kuridhisha kwa timu yake.
 Hapa alitamani hata aingie yeye uwanjani, auweke kwapani mpira na kutupia langoni mwa wapinzani wake.
Hapa akiwa na sura ya kukataa tamaa na kukubali yaishe baada ya dakika kuyoyoma bila Yanga kuambulia kitu. Picha hizi ni katika michezo ya Yanga walipokutana na mahasimu wao Simba.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment