Badhi ya majaji katika mashindano ya chemsha bongo kwa
wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam yaliyoandaliwa na
Taasisi ya An-Nahl , kutoka kushoto ni Mtoka Fikirini, Katibu wa vijana wa
taasisi hiyo, Abdulkarim Kichechele na Meneja Matukio, Baruani Fikirini.
Viongozi
wa Taasisi ya An-Nahl wakifuatilia maswali ya wanafunzi katika mashindano ya
chemsha bongo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mbaraka Maseneke, Amir wa Vijana Anthony Mahimbila, Mratibu
wa Habari, Farid Mbaraka na Mweka Hazina wa taasisi hiyo, Andallah ndelele,
mashindano hayo yamefanyika katika msikiti wa Kichangani, uliopo Magomeni.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari za
jijini Dar es Salaam, wakifuatilia maswali yanayoulizwa katika mashindano hayo
ya chemsha bongo.
TAASISI
ya An-Nahl imezindua mashindano ya chemsha bongo kwa wanafunzi wa shule za
sekondari, huku ikwashauri wanafunzi wengi kushiriki mashindano mbalimbali
yenye lengo la kuwasaidia katika kuongeza ufikiri na kupanua wigo wa mawazo.
Ushauri
huo umetolewa na Amir wa Vijana wa taasisi hiyo, Anthony Mahimbali wakati
akifungua mashindano hayo ambapo ameeleza kuwa, lengo la kuanzisha mashindano
hayo ni kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua
changamoto zao wenyewe.
Amesema,
masindano hayo kwa sasa mashindano hayo yanashirikisha shule za jiji la Dar es
Salaam pekee lakini wanajipanga kuhakikisha wanawafikia vijana wote nchini.
“Mashindano
haya hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, safari hii
tumealika shule karibu 200 ambazo ni za serikali na binafsi, kwasababu
mashindano haya si tu kwa ajili ya kujifunza dini lakini kuongeza uelewa kwa
sababu yanaulizwa maswali tofauti,” alisema Mahimbali.
Mahimbali
amesema, katika mashindano hayo wanafunzi huulizwa maswali ya papo hapo
yanayohusu dini, masomo ya darasani na mazingira ya jamii kwa ujumla ili kutoa
fursa kwa vijana hao kuchanganua mambo mbalimbali na kuongeza wigo wa kufikiri.
Amefafanua
kutokana na mashindano hayo kuhusisha maswali ya darasani yamewasaidia wanafunzi
wengi kusoma na kukumbuka kuhusu masomo yao, hatua ambayo imewasaidia katika
kuongeza ufaulu katika masomo yao.
Mchujo
wa mashindano hayo katika ngazi ya wilaya unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ambapo
umegawanywa katika wilaya tatu ambazo ni Kinondoni, Ilala na Temeke ili kupata
shule 15 zitakazoungana na bingwa mtetezi katika fainao itakayofanyika Juni 17
katika ukumbi wa city garden, Gerezani.
Mchujo
huo ambao katika wilaya ya Ilala utafanyika katika shule ya Seminari ya Ilala
Islami, Kinondoni shule ya sekondari Ridwaa na Temeke katika Chuo Kikuu cha
Elimu Dar es Salaam (DUCE).
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment