Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM
Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama,
kwa Mkoa wa Dar es Salaam,jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo, akiwasili kwenye Ukumbi wa Kijichi Mbagala kwa ajili ya kuzungumza na wanachama na Viongozi wa CCM.
Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogolo akiwasili ukumbini (kushoto) ni Mkubwa Fela akiwa ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano huo.
Wanachama wa CCM wakiimba wimbo maalum
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es Salaam,jana.
Vijana wa Kikundi cha Hamasa cha CCM Kata ya Mtoni, wakisebeneka wakati wa mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo, alipokuwa katika ziara ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es Salaam,jana.
Baadhi ya Wanachama wa CCM Kata ya Mtoni wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo,
Wazee wa CCM wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo, katika Ukumbi wa CCM Mtoni.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo, akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Mtoni kwa ajili ya kuzungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es Salaam,jana.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, wakati alipomtembelea ofisini kwake alipokuwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza kutoa shukrani zake kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala (hawapo pichani) kwa mapokezi, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwa Jimbo la Temeke jana.
Picha ya pamoja baada ya mazungumzo
Naibu akiagana na baadhi ya Viongozi ofisini kwa Mkuu wa Wilaya
*********************
*********************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick
Mpogolo,amesema hakuna mtu anayeweza kukinunua Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa ni
Chama kikubwa kilichoanzishwa na waasisi makini.
Amesema waasisi walizingatia
misingi ya haki umoja na mshikamano ,wakaondoa dhulma, chuki na ubaguzi wa kila
aina hivyo si rahisi mtu kufanya biashara na CCM.
Mpogolo alisema hayo jana
alipozungumza na viongozi na wanachama wa CCM katika majimbo ya Temeke na
Mbagala jijini Dar es Salaam,ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kuimarisha
Chama.
Alisema CCM inaendesha
shughuli zake kwa uhuru na itahakikisha uchaguzi wake unafanyika kwa haki
pasipo kuingilia na wanachama wenye tabia ya kununua madaraka.
Mpogolo aliwaagiza watendaji
wa Chama na jumuiya kusimamia uchaguzi
unaendelea kufanyika kwa haki bila kuwashinikiza wanachama kwa kuwa
wanawafahamu viongozi wanaowataka.
"Hatutaki vurugu CCM,
tunapenda amani,umoja na mshikamano. Wenye ni ya kutumia uchaguzi huu kupanga
mitandao yao, wataambulia patupu,watatumia fedha na uongozi
hawatapata,"alisema.
Aliwaonya wenye nia ya
kuwagawa wanachama kwa misingi ya udini na ukabila kuacha mara moja kwa kuwa
CCM haina dini wala kabila na wanachama wako huru kuchagua kiongozi anayefaa
bila kujali dini wala kabila yake.
Akizungumzia mabadiliko ndani
ya Chama, Mpogolo alisema yanalenga kurejesha nguvu ya Chama kwa wanachama ,kwa kujenga mashina yenye nguvu
huku balozi akiwa jukumu kubwa kuisimamia serikali.
Alisema mabadiliko hayo
yanataka kwenye shina kuwe na wanachama 50 hadi 150 ili kuongeza nguvu ya Chama
. Aliwataka wanachama na viongozi kujenga umoja,upendo ili wawe kivutio kwa
wengine wajiunge na CCM.
"Katika ziara yangu
nilifika Namtumbo nikakaribishwa nyumbani kwa balozi, akiwa na wanachama wake
50,akanieleza kwamba wana kero ya maji ,nikamsimamisha diwani aeleze mipango ya
kutatua kero hiyo.Pale ndio niliona nguvu ya balozi,"alisema.
Wakizungumza baada hotuba hiyo
,baadhi ya wanachama na viongozi walimshukuru Mpogolo kwa ziara hiyo
iliyosheheni mikakati ya kukijenga Chama na kuwaonya watendaji jambo ambalo.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Dar
Es Salaam, Saad Kusilawe, alisema Chama kimejipanga vizuri kukomboa majimbo
yote ya mkoa huo, hivyo ziara yake imeongeza nguvu kwenye mikakati inayoendelea
kutekelezwa.
Alisema kutokana na ziara hiyo
,anaamini uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu bila malalamiko wala
upendeleo na kila ngazi itapata viongozi bora watakaoshirikiana na
wanachama kukivusha Chama kwenye
uchaguzi ujao.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar
es Salaam,Janneth Masaburi, alisema ziara hiyo itasaidia kuwajenga kisiasa ili
waendane na kasi ya mabadiliko ya ujenzi wa Chama na kasi ya Mwenyekiti wa CCM,
Rais Dk. John Magufuli.
Alisema Mpogolo amegusa mambo
muhimu, ambayo yatasaidia wanachama kufanya uchaguzi huru na viongozi wa mkoa
wataendelea kuelimisha wana CCM ili kujiimarisha zaidi.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam Mariam
Kisangi, alisema Naibu Katibu Mkuu Mpogolo, anatoa elimu muhimu juu ya dhamira
ya Chama ya kujenga mashina na kuongeza wanachama.
Alisema ziara hiyo imejenga
hamasa na wanachama wameelimishwa kuepuka chuki na kujenga upendo miongoni mwao
jambo ambalo ni muhimu hususan kwa kipindi cha uchaguzi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment