Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 12 April 2017

TTB NA CLOUDS MEDIA WAENDESHA KAMPENI YA “TALII NA TTB” MSIMU HUU WA PASAKA.

 Mkurugenzi wa Bodinya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi
 Watangazaji wa kipindi maarufu cha 360 cha Clouds Tv watakao safari na timu nzima ya Clouds Tv, washindi wa shindano katika kampeni ya  Talii na TTB’ pamoja na maofisa wa TTB katika ziara ya kutembelea vivutio vya utalii vya kaskazini ya Tanzania.
Na Geofrey Tengeneza
Katika mkakati wa kukuza utalii wa ndani  (Domestic Tourism) Bodi ya Utalii Tanzania - TTB kwa kushirikiana na Clouds Media Entertainment  inaendesha Kampeni Maalumu iitwayo ‘Talii na TTB’ katika msimu huu wa Pasaka kwa lengo la kuhamasiha watanzania  kutembelea vivutio vyetu mbalimbali vya utalii hapa nchini.

Akizungumza leo katika Kipindi cha 360 cha Clouds TV Mkurugenzi Mwendeshaji  wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi  amesema kuwa katika Kampeni hiyo timu ya watangazaji wa 360 na mafundi mitambo wa Clouds TV wakiambatana na maafisa wa Bodi ya utalii wataondoka jijini Dar es salaam tarehe 13/04/2017 kwa shirika la ndege la ATCL kwa  ziara ya kutembelea baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo kaskazini mwa Tanzania.

Amesema kuwa katika ziara hiyo iliyoandaliwa na Bodi ya utalii Tanzania, sambamba na timu hiyo ya 360 watakuwemo pia washindi wanne (4) wa shindano maalumu katika kampeni hiyo lililoendeshwa na TTB kwa kushirikiana na 360, ambao watasafiri kwa kutumia shirika la ndege la Tanzania (ATCL) kutoka Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) na baadae kusafiri kwa magari kueleka Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro, Olduvai Gorge, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ambako pamoja na mambo mengine Clouds TV kupitia kipindi chake 360 watarusha mbashara matangazo yake kutoka maeneo hayo ya vivutio vya utalii kwa siku hizo zote watakazokuwa huko.

Akizungumzia washindi waliopatikana Bi Devota Mdachi amesema kuwa TTB kwa kushirikiana na 360 ya Clouds TV waliendesha shindano la kuwapata washindi kwa kuiwataka wananchi kutuma picha yeyote anayoiona kuwa ni nzuri inayomuonesha akiwa katika moja ya kivutio cha utalii ambapo washindi picha mbili bora zilipatikana na kila mshindi amezawadiwa safari hiyo ambayo ataambatana na mwenzi wake.  

Amewataja walioshinda na kuzawadiwa safari hiyo ya siku tano itakayogharimiwa na TTB kuwa ni:
Magoti H. Mtani na mwenzi wake Bi Jamila Y. Massawe
Mvumo A. Balati na mwenzi wake Bi Getrude R. Mnaye
Amewashukuru wadau mbalimbali waliosaidia kufanikisha safari hiyo ambao ni pamoja na TANAPA, NCAA, ATCL, Burudica Lodge, Serengeti Safari Camp, na  Ngorngoro Farm Lodge.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment