Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 29 April 2017

SOKO LA MWEMBE TAYARI DODOMA LATEKETEA KWA MOTO

 Wafanya biashara katika soko la wauza vifaa chakavu vya magari na mitambo pamoja na vya ujenzi la Mwembe Tayari mjini Dodoma wakifarijiana baada ya soko hilo kuteketea kwa moto lote usiku wa kuamkia leo.
 Nimajonzi tupu kwa wafanya biashara soko la Mwembe Tayari hasa ukizingatia kua biashara nyingi siku hizi mitaji yake ni mikopo toka taasisi za fedha.
 Wananchi wakiangalia mabaki.
Chanzo cha moto inaamini ni mmoja wa akina mama ntilie ambao hua na tabia ya kubandika maharagwe na kuyaacha yakiendelea kuiva usiku kucha bila uangalizi wowote.
Na Urban Epimark, Dodoma.
SOKO la wauza vifaa chakavu vya magari na mitambo pamoja na vya ujenzi la Mwembe Tayari mjini Dodoma limeshika moto na kuungua lote usiku wa kuamkia leo.

Soko hilo lililopo makutano ya barabara ya kuelekea Singida lenye wafanyabisha mchanganyiko ambao ni wajasiriamali, hua ni mkombozi mkubwa kwa watu tofauti mjini Dodoma.

Naibu Mwenyekiti wa Soko hilo Bw Aloyce Emanuel Mboro, ameeleza idadi ya mabanda yalitoungua ni takribani 80 na yenye mali, ambapo hakuweza kutoa makadirio ya thamani yake.

Nae mhanga aliyeunguliwa banda lake Bw Salvatory Joseph Shio akieleza kwa uchungu kwamba banda lake limeungua lote, na lilikuwa na mali yenye thamani ipatayo millioni 30 na amekopa benki, ana familia na anasomesha watoto, hajui cha kufanya.

Salvatory ameeleza pia chanzo cha moto inaamini ni mmoja wa akina mama ntilie ambao hua na tabia ya kubandika maharagwe na kuyaacha yakiendelea kuiva usiku kucha bila uangalizi wowote.

Inasemekana ni vipande vya cheche za moto, ziliruka na kushika banda moja na kupeperushwa na moto na kuenea kwingine.

Aidha, walinzi wenye kulinda soko hilo ambao wapo nane, wote walikimbia kujificha ili kuhofia hamaki na hasira za wafanyibiashara.

Huduma ya Zimamoto, inavyosemekana walifika sokoni hapo majira ya saa 06:30 usiku, moto ulikuwa mkubwa na hawakuweza kuudhibiti, badala yake walilinda kituo cha mafuta kilichopo jirani ili moto usilete madhara zaidi.

Hakuna afisa yeyote wa serikali aliyeweza kupatikana asubuhi hii wala Diwani wa eneo hilo, bali wahanga wameiomba serikali iwaangalie kwa jicho la huruma ili waweze tena kuyamudu maisha.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment