Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa
(kushoto), wakisaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya anga baina ya
nchi hizo mbili, jijini Arusha
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa (kulia), akibadilishana hati za makubaliano na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), kuhusu ushirikiano katika masuala
ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri
wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakionesha hati zao za
makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo, jijini
Arusha Aprili 5,2017. Mkataba huo utaimarisha huduma za usafiri na usalama wa anga.
Akizungumza
mara baada ya kusaini mkataba huo jijini Arusha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mkataba huo utaruhusu ndege za nchi
hizo mbili kutua na kuruka bila vikwazo vyovyote katika nchi hizo.
"Naamini
ushirikiano huu utaboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka za usafiri wa Anga na
hivyo kuongeza viwango vya usalama wa usafiri huu", amasesema Prof. Mbarawa.
Naye
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesisitiza kuwa mkataba
huo ni muendelezo wa ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Uganda na hivyo
kuchochea maendeleo ya uchumi kwa raia wa nchi hizo.
Ushirikiano
wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya mkakati wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika kuwezesha wananchi wake kunufaika na fursa za kijamii,
kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment