Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday 19 April 2017

CHANGAMOTO ZITOKANAZO NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA.



SERIKALI imesema kuwa  imechukua  hatua  mahsusi katika kukabiliana na changamoto zinazotokana  na Agenda ya Mabadiliko ya Umoja wa Ulaya.

Akifafanua hoja hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Suzan Kolimba amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali ambazo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kusimamia matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha tunapunguza utegemezi kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Pia Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia Sera ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi ya mwaka 2009 na sheria ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi ya mwaka 2010. Imebainishwa kuwa mkakati huu unasaidia kuongeza wigo wa vyanzo za fedha za kugharamia miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi kwa wahisani.

Hata hivyo Serikali inaendelea kuwashawishi wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza zaidi nchini na zinaenda sambamba na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara nchini na kupunguza gharama za kufanya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini.

Katika kuratibu uhamasishaji wa watanzania waishio ughaibuni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeanzisha Idara maalum ya kuratibu masuala ya Diaspora ili kushiriki katika Maendeleo ya Nchi ikiwemo kuwekeza nchini.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment