Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 2 March 2017

UDOM YATENGENEZA MFUMO WA KUHAKIKI TAARIFA NA HOTUBA KUWABANA WAHALIFU WA MTANDAO



Na Katuma Masamba


CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetengeza mfumo wenye uwezo wa kuhakiki taarifa na hotuba mbalimbali na kubainisha kama ni halisi au zimechezewa na wahalifu wa kimtandao.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitivo cha Elimu Ang’avu wa UDOM, Profesa Leonard Mselle katika semina ya juu ya utafiti wa masuala ya usalama wa mtanadao ambapo alisema, mtambo huo unaweza kuonesha kama taarifa ni sahihi au imechezewa.

Awali Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi alisema, suala la usalama wa mtandao ni jambo muhimu hasa kwa kuzingatia teknolojia inakua kila siku.

Alisema kama hakutakuwa na usalama juu ya mitandao kuna hatari mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na matumizi ya mtandao.

“…Kutokana na teknolojia ambazo zipo na nia ya serikali ya kuwekeza kwenye tafiti, leo tumeona mbinu au mifumo mbalimbali inayotengzwa hapa nchini kwa ajili ya kutulinda katika matumizi ya mtanadao,” alisema Dk Yonazi.

Profesa Mselle alisema, mtambo huo una uwezo wa kuanisha taarifa kama ni halisi ambapo ukiweka tyaarifa au hotuba unayotaka kubaini ukweli wake itaonesha kama ni halisi au imechezewa.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment