Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday 17 March 2017

TUNDU LISSU AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU ASHITAKIWA KWA MAKOSA MATANO

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (kulia) akisubiri kuingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mbele ya Hakimu Mkazi, Respicious Mwijage kusomewa mashitaka yanayomkabili.
 ***************
Na Francisca Emmanuel
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo kutoa maneno yenye nia ya kuumiza hisia za kidini.

Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja Nchimi amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Respicious Mwijage kuwa mashitaka hayo yamefanyika Januari 11, mwaka huu huko Kondeni wilaya ya Magharibi B mkoa wa Magharibi B huko Zanzibar wakati wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Dimani.

Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na upande wa mashitaka uliomba kumsomea mshitakiwa maelezo ya awaHata hivyo, Hakimu Mwijage alisema kabla ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali ni lazima wajue kuhusu maombi ya dhamana kisha ndio wataendelea

Lissu ambaye anajiwakilisha mwenyewe, ameomba dhamana kwa kuwa kuna uchaguzi wa Chama cha Mwanasheria Tanganyika (TLS) unaofanyika leo na kesho na kwamba yeye ni mgombea Urais na kwamba Jaji Mkuu ametoa barua kwa Mahakama zote kuwataka mawakili kuhudhuria uchaguzi huo

Pia alidai mashitaka yote kasoro hilo la kwanza yaliwahi kusomwa mahakamani hapo na alipatiwa dhamana hivyo apatiwe dhamanaNchimbi amesema DPP hajaona sababu ya kuweka pingamizi la dhamana kwa mshitakiwa kwa sababu mashitaka yanayomkabili Lissu yanadhaminika


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment