Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Friday, 17 March 2017

MKUU WA MKOA MBEYA AKAGUA UWANJA WA NDEGE SONGWEMkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitembelea maeneo mbalimbali
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi ya uwanja wa Ndege wa Songwe uliopo mkoani humo.
Makalla amekagua ujenzi huo na kuonesha kufurahishwa na mkandarasi  kurejea na kuendelea na kazi ya ujenzi wa jengo la abiria ambalo lilisimama kwa muda.

Katika ziara hiyo Makalla maetembelea na kukagua jengo la  kituo cha polisi uwanja wa Ndege Songwe na miundombinu mingine ambayo ilikuwa haija kamilika.

Vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja huo vimemhakikisha Mkuu wa Mkoa Amos Makala jinsi vilivyojipanga katika kuhakikisha vinadhibiti mianya yote ya upitishaji dawa za kulevya katika uwanja huo.

Pamoja na mambo menginre Mkuu wa Mkoa ameeleza mipango iliyopo ya matumizi ya uwanja wa ndege wa Songwe na namna uwanja huo utakavyokuwa lango la biashara na utalii kwa nchi Nyingi za kusini mwa Afrika.  

“Uwanja huu utakuwa si moja ya njia ya rahisi za usafiri kwa wakazi na wageni wajao Mkoani mbeya lakini uwanja wa Songwe utachochea uchumi kwa wananchi wa Mbeya, mikoa jirani na watanzanzania kwa ujumla,”alisema Makalla.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment