Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 11 March 2017

RAHCO WAANZA BOMOABOMOA YA WAVAMIZI WA RELI DAR ES SALAAM

Tingatinga likibomoa nyumba ambazo zipo ndani ya hifadhi ya reli katika eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam leo. Nyumba zote zilizondani ya hifadhi ya reli umbali wa mita 30 zimeanza kubomolewa kuanzia alfajiri ya leo. (Picha na Mroki Mroki).

Na Mroki Mroki

KAMPUNI Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco) kupitia kampuni ya udalali ya Heputwa Investment leo imebomoa nyumba za makazi na biashara zilizo ndani ya mita 30 kutoka ili reli.

Bomoabomoa hiyo anafanywa kukiwa na ulinzi wa polisi wenye magari ya maji ya kuwasha, silaha zikiwemo bunduki zenye risasi za moto na mabomu ya machozi.

Meneja Uendeshaji wa Hepautwa, Idd Kebwe amesema wanatekeleza kazi waliyopewa na mteja wao na kwamba, wahusika walishapewa taarifa.

“Tulishatoa taarifa juu ya kazi hii inayofanyika hii leo kwa kutoa ilani ya kuwataka watu wahame lakini pia hatukuishia hapo tulitoa taarifa ya kubandika matangazo na pia kupita na gari na kipaza sauti kuwa leo tutaendesha bomoabomoa,”amesema Kebwe.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Buguruni Madenge ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Buguruni kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Adam Mfugame amesema notisi waliyokuwa wamepewa ni ya wananchi kubomoa nyumba zao zilizo ndani ya mita 15 na si mita 30.

“Notisi tuliyonayo ni ile iliyotolewa Julai 4, 2016 ambayayo iliwataka wananchi kubomoa makazi yao yaliyondani ya mita 15 na walifanya hivyo lakini leo kilichofanyika ni uvamizi kwani watu hawa hawajatoa taarifa ofisi yeyote kuanzia mtaa hadi kata kuwa wanabomoa mita 30,” amesema Mfugame.

Rahco baada ya kutoa notisi ya siku 30 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliovamia maeneo ya reli Julai 4, 2016 siku inayofuata ilianza kuziwekea alama X nyumba zilizopo ndani ya eneo la reli.

Ubomoaji wa leo inadaiwa kufanyika kwa kuzingatia Sheria ya Reli Na.4 ya Mwaka 2002 inayokataza watu kujenga karibu na njia za reli.

Kifungu cha 57(2) cha shera hiyo kinakataza wananchi kuvamia maeneo ya reli,  na  katika kifungu cha nne kimeainisha umbali, kwa mjini mita 15 na vijijini mita 30.

Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Dk Mussa Mgwatu aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa tathmini za maeneo hayo zilifanywa tangu Machi 2016 na ilipofika Aprili 25, 2016, walitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari wakiwataka wananchi wabomoe nyumba zilizo kwenye hifadhi ya reli.

 Polisi FFU wakilinda Doria eneo la bomoabomoa.
 Tingatinga likibomoa nyumba ambazo zipo ndani ya hifadhi ya reli katika eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam leo. Nyumba zote zilizondani ya hifadhi ya reli umbali wa mita 30 zimeanza kubomolewa kuanzia alfajiri ya leo. (Picha na Mroki Mroki).

 Mkazi wa Buguruni akiwa na mizigo yake kando ya reli baada ya kukumbwa na bobomoa ya RAHCO hii leo.
 Ulinzi mkali eneo hilo.
Treni ya Ubungo ikipita eneo ilipokuwa inafanyika bomoabomoa


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment