Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday 10 March 2017

DODOMA MJINI WAZINDUA KAMPENI YA MAGAUNI MANNE KWA WATOTO WA KIKE

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,  Anthony Mavunde akisalimiana na mmoja wa wanafunzi aliyeshiriki katika uzinduzi wa magauni manne mjini Dodoma.
Naibu Waziri Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la dodoma mjini, akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme.


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,  Christina Mndeme kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya vijana Dodoma (DOYODO) na wadau wengine amezindua kampeni ya Magauni Manne kwa Wasichana yenye lengo la kupambana na mimba za utotoni kwa wasichana waliopo katika masomo kwa shule za Msingi na Sekondari.

Kampeni ya magauni manne inalenga kuhamasisha Wasichana waliopo katika Masomo (#Vipepeo) kupata elimu, kuhitimu, kuingia katika ndoa na hatimaye kuwa na familia katika mtiririko unaofaa bila ya kuruka hatua yeyote huku pia ikilenga kuwaasa mabinti kuepukana na vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zao.

Magauni manne ni lugha ya picha inayosimama kumaanisha hatua anazopitia binti #Kipepeo kuanzia akiwa shuleni mpaka kuolewa
•Gauni la kwanza Sare ya Shule
•Gauni la pili Joho la Mahafali
•Gauni la Tatu Gauni la Harusi
•Gauni la Nne Gauni la wakati wa ujauzito (Maternity)

Akizungumza katika uzinduzi huoMkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Mndeme amesema kwa mwaka 2016 wanafunzi 6 wa Shule za msingi walibainika kupata ujauzito huku kwa Shule za Sekondari Wanafunzi 58 wakibainika kupata ujauzito wakati kwa mwaka 2017 pekee kuanzia Mwezi Januari mpaka mwezi wa Machi wanafunzi 18 tayari wamebainika kuwa na ujauzito

Uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Dodoma ulihudhuriwa na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,  Anthony Mavunde pamoja na Mbunge wa Viti Maalum (Dodoma) Mhe. Felista Bura.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment