Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 16 January 2018

SERIKALI YAWAPONGEZA WASHINDI WA TUZO ZA KIMATAIFA ZA KISWAHILI YA MABATI -CORNELL YA FASIHI YA AFRIKA 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe,  amewapongeza Dotto Rangimoto na Ali Hilal Ali kwa kushinda tuzo za mashindano ya Kimataifa ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika ya mwaka 2017 yanayoandaliwa na Chuo Kikuu cha Cornell nchini Marekani kwakushirikiana na Kampuni ya ALAF Ltd yaliyofanyika jana Januari15, 2018 mjini Newyork.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa ushindi wa Watanzania hawa ni ushindi wa Taifa kwa ujumla, hivyo kwa niaba ya Serikali anawapongeza sana kwakutangaza utamaduni wetu kupitia lugha ya Kiswahili na kuipeperusha bendara ya Taifa letu Kimataifa. 

Amesema ushindi wa Dotto na  Ali unachagiza juhudi za Serikali za kuibidhaisha lugha ya Kiswahili.

Tuzo za Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika zenye lengo la kutambua na kukuza vipaji vya uandishi kwa lugha za Kiafrika, kuhimiza sanaa ya tafsiri baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe na kutafsiri maandishi ya lugha nyingine kwa lugha za Kiafrika zili asisiwa mwaka 2014. 

Tuzo hizi huandaliwa kila mwaka ambapo washiriki mbalimbali kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki hushiriki. Katika tuzo za mwaka 2017, Dotto Rangimoto ameshinda tuzo katika kipengele cha uandishi wa Ushairi na Ali Hilal Ali ameshinda tuzo katika kipengele cha uandishi wa Riwaya.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment