Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, 27 March 2017

POLISI WATEKELEZA AGIZO LA KUMWACHIA HURU NEY WA MITEGO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamemwachia huru Msaanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki maarufu Ney wa Mitego.

Polisi wamemwachia huru msanii huyo jioni ya leo ikiwa ni muda mfupi baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harison Mwakyembe kuliagiza jeshi hilo kumwachia huru msaani huyo huku akiiomba Baraza la Sanaa la Taifa lililokuwa limeagiza kushikiliwa kwake na kuzuia upigwaji wa Mziki wake mpya wa 'WAPO' pia iuruhusu wimbo huo kupigwa katika vituo vya redio na maeneo mengine.

Msanii Ney alikuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kumkamata juzi mkoani Morogoro na kumsafirisha hadi jijini Dar es Salaam kufuatia amri ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kile kilichodaiwa ni wimbo huo kukosa maudhui na kukiuka sharia za Basata.

Waziri Mwakyembe alifuatilia sakata hilo la kukamatwa Ney na baadae Basata kufahamisha sababu za kumkamata na kutakiwa kuhojiwa juu ya nyimbo yake ya ‘Wapo’ lakini pia Rais alimuagiza kufuatilia suala hilo na kuona namna ya kulimaliza kwakuwa haoni kosa katika wimbo huo.

Aidha Mwakweye amesema Rais Magufuli aliomba Ney achiwe hivyo nayeye akiliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru msanii huyo.Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment