Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 14 March 2017

MAKONDA AAMURU NYUMBA 36 ZILIZOJENGWA KANDOKANDO YA BONDE LA MTO MSIMBAZI KUVUNJWA IFIKAPO KESHO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi waliokumbwa na mafuriko  katika maeneo  ya Mnyamani na Tabata Kando Kando ya Bonde la Mto Msmbazi kutokana mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akitoa neno kwa wananchi walifikwa na mafuriko katika eneo la myanyamani kando kando ya bonde la Mto Msimbazi leo jijini Dar es Salaam.
************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Pau Makonda amesema nyumba 36 zilizojengwa kando kando ya Mto Msimbazi zianatakiwa kuvunjwa kesho kutokana  nyumba hizo zilishakuwa zimelipwa katika mafuriko  yaliyopita.

Akizungumza na wananchi waliopata mafuriko jana, Makonda amesema watu walipewa viwanja mabwepande waishindwa kuvunja ili waweze kupangisha kutokana na kuwa na akili nyingi lakini dawa yake ni kesho  kuzivunja.

Makonda amesema kuwa kuna mpango wa kupata fedha kutoka benki ya dunia zitapanua mto ambazo serikali ya Tanzania italipa fedha hizo na kuongeza kuwa watu ambao wamejenga kandokando ya mto msimbazi.

Amesema kuwa wakati wa matatizo ya mafuriko wanajitokeza kwa wingi lakini mikutano ya kawaida mahudhurio hafifu hali hii lazima watanzania tuondokane.

Aidha amesema kuwa serikali inapoteza fedha nyngi kwa  ajili ya kusaidia watu wenye maafa bila kujua fedhahizo ni za kodi ambazo zinatakiwa zifanye shughuli za maendeleo  bila kujali watu wanaona fedha  hizo zinatolewa  mbinguni ambapo ni ndoto.

 Makonda amesema kuwa watu wanaojenga nyumba kuanzia msingi wanaonekana lakini wananchi wanashindwa kusema mpaka mafuriko yanaingia ndani ndio wanajua mafara ya nyumba kujenga katika mkondo wa mto.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuna watu watafidia wale watu ambao kweli wanatakiwa kufidiwa na sio wale waliohamishwa wakarudi tena .
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakiangalia eneo la Mnyamani na Tabata jinsi lilivyoathirika na mafuriko ya jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akivuka katika kivuko cha watembea kwa miguu kwenda kuangalia wananchi walioadhirika na mafuriko leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisaidiwa na kuvuka kuwenda upande wapili katika eneo la Mnyamani na Tabata kando kando ya Bonde la Mto Msimbazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakiangalia eneo la Mnyamani na Tabata jinsi lilivyoathirika na mafuriko ya jana.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment