Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Sunday, 5 March 2017

MAGUFULI ATOA SIKU 7 DANGOTE APEWE ENEO

Na Basil Msongo
RAIS John Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini impe mfanyabiashara Aliko Dangote eneo la kuchimba makaa ya mawe na agizo hilo liwe limetekelezwa ndani ya siku saba kuanzia leo.

Ameiagiza kuwa, makaa ya mawe yakiisha kwenye eneo atakapopewa Dangote, apewe eneo lingine.

Ametoa maagizo hayo leo mkoani Mtwara kabla ya kuzindua magari 580 ya Dangote yatakayokuwa yakibeba saruji kutoka kiwandani.

“Nia yangu nataka kiwanda hiki kifanye kweli ili ikiwezekana ujenge viwanda vingine…ujenge hata kumi” amesema Rais Magufuli.

Amemruhusu Dangote auze makaa hayo kwa watu wengine ili Serikali ipate fedha.
Ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kukusanya mapato ya uchimbaji wa makaa hayo kwa Dangote mwenyewe.

Rais amemhakikishia Dangote kuwa, ndani ya siku saba atakuwa amepata kibali cha kuchimba makaa ya mawe kwa ajili ya kiwanda cha saruji kilichopo Mtwara.

Ameiagiza menejimenti ya kiwanda cha Dangote iwasiliane na serikali moja kwa moja badala ya kupitia kwa watu wengine.

Rais amesema, dunia inakwenda haraka sana hivyo uamuzi kuhusu changamoto zilizopo lazima ufanywe haraka ili Tanzania iendane na kasi hiyo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment