Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 7 February 2017

KUANZIA MWEZI JUNI MWAKA HUU POMBE ZA VIROBA MARUFUKU NCHINI

 Serikali imesema Bungeni kua kuanzia mwezi Juni mwaka huu itapiga marufuku uzwaji wa pombe zote katika viroba.

Akizungumza Bungeni mjini Dodoma wakati wa kujibu hoja za wabunge kufuatia michango mbalimbali yao juu ya hoja za Kamati za UKIMWI na Madawa ya Kulevya na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya jamii. , Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala, alisema itapiga Marufuku Matumizi ya Pombe za VIROBA Kufikia Mwezi wa Sita mwaka 2017. 

"Serikali kuzuia viroba kutengenezwa nchini na kufuta kabisa matumizi ya pombe za aina ya viroba ndani ya nchi yetu,"alisema Dk Kingwangala.

Dk. Kigwangalla alisema, haitopita mwezi wa sita Serikali itakuwa imepiga marufuku matumizi ya madawa ya kulevya nchini.

Miezi kadhaa iliyopita Dk. Kigwangalla aliongoza kikosi kazi cha Serikali kilichokuwa kinashughulikia suala la viroba ili kutathmini ukubwa wa tatizo na kupendekeza hatua za kuchukua. 

Kikosi kazi kilibaini changamoto nyingi ikiwemo ya uwepo wa viwanda bubu na pombe zinazochanganywa na spirit ya viwandani.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment