Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika kutoka nchini Marekani kwa mara ya
kwanza wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization Procedure) kwa
mgonjwa na kuzibua mshipa wa Moyo uliokuwa imeziba kwa zaidi ya miezi mitatu (kwa lugha
ya kitaalamu Chronic Total Occlusion).
Upasuaji
huo ambao unatumia mishipa ya damu ulichukuwa muda wa saa moja kwa kuzibua mshipa mmoja wa damu ambao ulikuwa
umeziba kwa asilimia 100 na kushindwa kupeleka damu upande wa kushoto wa moyo.
Kambi
ya Madakari wa Afrika imeanza tarehe 23/1/2017 na inatarajiwa kumalizika tarehe
29/1/2017. Hadi sasa jumla ya wagonjwa sita
wameshapatiwa huduma za matibabu ya moyo ambayo ni kuzibua mishipa ya moyo
iliyokuwa imeziba. Hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na wanatarajiwa kuruhusiwa
siku yoyote kuanzia kesho.
Tangu
kuanza kwa mwaka huu wagonjwa 29 wameshafanyiwa
upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya wagonjwa hao 23 wamefanyiwa upasuaji
katika kambi za ndani na wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya
Madaktari Afrika.
Taasisi
inaendelea kuwaomba Madaktari wote
nchini wenye wagonjwa wao wa matatizo ya moyo wawatume wagonjwa hao katika Taasisi ya
Moyo ili waweze kupatiwa matibabu. Kwa
mawasiliano zaidi wawasiliane na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502
na 022-2151379 ambaye atawaelekeza utaratibu wa kuwatuma wagonjwa hao.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment