Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF)Dk. Reginald Mengi akizungumza jijini Dar es salaam jana wakati akitolea ufafanuzi juu ya baraza la kibiasha baina ya Uturuki na Tanzania lililoundwa juzi baaina ya taasisi hiyo na Bpodi ya mahusiano ya kigeni kwenye masuala ya kiuchumi nchini Utururuki (DIeK). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye (kushoto) akizungumzia uundwaji huo wa baraza la kibiashara baina ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Mwenyekiti wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF)Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana juu ya baraza la kibiasha baina ya Uturuki na Tanzania lililoundwa juzi baaina ya taasisi hiyo na Bpodi ya mahusiano ya kigeni kwenye masuala ya kiuchumi nchini Utururuki (DIeK).
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akifafanua jambo.
*************
Na Daily News/Habarileo Blog,
TAASISI ya Sekta
Binafsi (TPSF) imeanza mchakato wa kuunda sekretarieti ya Baraza la Kibiashara
baina ya Uturuki na Tanzania ili kwenda na kasi aliyoagiza Rais John
Magufuli ya kutaka kuongeza thamani ya
biashara baina ya Tanzania na Uturuki.
Kuundwa kwa baraza hilo kunatokana na makubalino
yaliyofanywa na Rais Magufuli na Rais wa Uturuki, Recep Erdogan kuongeza
thamani ya biashara baina ya Tanzania na Uturuki kutoka dola za Marekani
milioni 190 hadi kufikia dola za Marekani milioni 250.
Akizungumza jana na waandishi wa habari,
Mtendaji Mkuu wa PSPF, Geoffrey Simbeye alisema Baraza hilo linaundwa na TPSF
na Taasisi Binafsi ya Uturukli (DEiK) na limeundwa jana wakati wafanyabiashara
wa pande mbili walipokutana.
Alifafanua kuwa DEiK itaunda Sekretreti ya
Upande wa Uturuki na TPSF itaunda sekretarieti kwa upande wa Tanzania.
Alifafanua kuwa baraza kuu la biashara litahusisha sekta mbalimbali za nchi
hizombili na kuendelea kuangalia uwezekano wa ushirikiano zaidi kwa manufaa ya
nchi hizo mbili.
Alisema kamati ndogo za baraza zinatarajiwa
kukutana angalau mara moja kwa mwaka, kutazama na kujadili mafanikio ya baraza
kwenye masuala ya kibiashara,uwekezaji, teknolojia baina ya Uturuki na
Tanzania.
Alitaja kazi za baraza hilo itakuwa ni kusaidia
kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili na kutoa mchango katika kuanzisha na
kukuza iwanda, kupitia ushirikiano wa teknolojia wa mashirika na tasisi za
kiuchumi za nchini uturuki.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa
TPSF, Reginald Mengi alisema Watanzania wanatakiwa kutumia fursa ya kuwepo kwa
baraza hilo ili kuongeza wigo wa kibiashara. Alisema Rais Magufuli amefanya
kazi yake ya kumleta Rais wa Uturuki pamoja na wafanyabiashara wa Uturuki.
"Kilichobaki ni kwetu sisi wafanyabiashara
sasa kuchangamkia fursa zilizopo kwa pande zote mbili. Tunatoa mwito kwa
wafanyabiashara wahakikisha hawapotezi fursa hii kwani imekuja wakati
muafaka," alisema Mengi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment